Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 130
- 368
Dj huyo ambaye alilelewa kwenye maisha yenye maadili ya dini huku mama yake akiwa ni mwana kwaya kanisani, alijitahidi kupigania muziki wa bongo fleva wakati unaanza nchini Tanzania, kwa kuwashika mkono wasanii mbali mbali, mpaka kufikia hatua ya kuwa wasanii wakubwa na kuitangaza bongo fleva.
Dj Bony Love, ametumia zaidi ya miaka 31 katika maisha yake katika tasnia ya muziki ikiwemo u-Dj na uandaaji wa muziki (producer), tangu bongo fleva inazaliwa na kuweza kusimama.
Dj Bonny Love alitumia muda, akili na nguvu zake katika kuinua sanaa ya Tanzania, kwa kutafuta wasanii na kuwapa fursa ya kurekodi bure, huku wasanii wengi wakubwa kwenye game ya bongo fleva wamepitia mikononi mwake, wakiwemo Juma Nature ambaye ndiye msanii anayesimama kama icon ya muziki wa bongo fleva, King Crazy Gk, mwana FA, Ay na wengineo.
Pia Dj Bonny love ni kaka wa maDj wakubwa wawili hapa bongo, wakiwemo Dj Venture na Dj Mackay. Tazama historia yake hapa chini
P Funk Majani
Paul Matthysse (maarufu kama P Funk, Halfani, Majani, Kinywele Kimoja, Mkono wa Mungu) ni mtayarishaji wa muziki na pia mmiliki wa Studio ya Bongo Records iliyopo jijini Dar es Salaam, Tanzania. Anaaminiwa na wengi kuwa ndiye mtayarishaji bora wa muda wote wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania.
P Funk ambaye ni nusu Mtanzania na nusu Mdachi, kama miaka ishirini iliyopita alikuwa na hisia za kupendelea muziki na pindi hadi kuamua kufanya kweli kuvutiwa kwake kupenda muziki ndio chanzo kikubwa kilichopelekea kufanikiwa katika muziki.
Kwenye miaka 1991-92 wakati bado yupo shule IST (International School Of Tanganyika). Alikuwa mtundu kwenye studio za pale shule kupigapiga midundo mbalimbali ya hapa na pale na kufoka-foka(Rap music) na pia alikuwa mbele sana kwa kupiga muziki kwenye pati mbalimbali na hapo alikuwa kupenda sana muziki kwa ujumla.
Joachim Marunda Msaafiri Kimaryo maarafu kama ‘Master J’ anatoka katika familia ya Watoto wawili , yeye akiwa wa kwanza na ana mdogo wa kike.
Kama mtayarishaji wa muziki hodari nchini Tanzania na mmiliki wa studio ya Muziki ya MJ Records, Master J amefanya kazi na kukuza vipaji vya wasanii wengi sana Tanzania.
Tangu mwaka wa 2007, Master J amekalia kiti cha mmoja wa majaji katika mashidano ya Bongo Star Search, ‘BSS’.
Kipindi hicho maarufu hakikuweza kutambulika peke yake bila ya Master J.
Kabla ya kukomaa kama producer mkuu nchini Tanzania, Master J amepitia mengi katika maisha yake binafsi na familia .
Master J akiwa mdogo ndoto yake kubwa ilikuwa kuwa rubani. Kutokana na utundu kupita kiasi Master J hakuwa anafanya vizuri darasani , mpaka pale walipo hamia Botswana.
Ndoto yake ili balilika wakati alikuwa huko huko shuleni ulaya aligundua anapenda sana ubunifu kuliko kitu kingine . na hapo ndipo alipo anzia kupenda kutayarisha muziki.
Mtu wa kwanza ktambulisha katika maswala ya muziki alikua mwanafunzi mwenzie Owen Shahada kutoka nchi ya Barbados ambaye alimfunza kucheza gitaa na kibodi.
Alirejea nyumbani mwaka wa 1996 na kufungua studio yake na kurekodi wimbo wake wa kwanza na bendi ya ‘the diplomats’.
Wakati Joseph Kusaga alipofungua kituo cha redio ilibidi Master J atafute njia mbadala ya kuwasilisha kazi zake kwenye jamii . Alijitahidi kuhamia mfumo wa digitali wa kurekodi.
Miikka Aleksanteri Kari (anafahamika zaidi kwa jina lake la kitayarishaji kama Miikka Mwamba; amezaliwa Helsinki, Ufini, 16 Oktoba 1971) ni mtayarishaji wa muziki na mhandisi wa sauti toka nchini Ufini-Tanzania. Miikka Mwamba ni mtayarishaji mashuhuri sana kwa nchi ya Tanzania, na ameweza kujibebea umaarufu mkubwa sana nchini Tanzania kunako miaka ya 2000.
Jina lake ni Miikka Kari, ila Kari alibadili iwe kwa Kiswahili na tafsiri yake ni Mwamba, hivyo aliamua kujiita Miikka Mwamba
Miikka aliwahi kufanya kazi na wasanii mbalimbali wa nchini Tanzania. Wasanii hao ni: Dully Sykes, Inspector Haroun, Lady Jay Dee, Mad Ice, Chegge, Mandojo na Domo Kaya, Solid Ground Family, Complex, Zahrani (maarufu kama Big Punisher wa Bongo), Only Face, Dknob na wengine wengi wa kutoka Tanzania.
Miikka alihitimu elimu yake ya msingi na sekondari Lohja, ambacho ni chuo cha sanaa (Torkkelin kuvataidelukio) alisomea Helsinki, na shahada ya uzamili (MA) alipata Theatre Academy of Finland, Dept. of Light and Sound Design.
Nyimbo zilizotamba
Julieta - Dully Sykes (2000)
Athumani Mlevi - Solid Ground Family (2001)
Baby Gal - Mad Ice (2002)
Tupa Mawe - Zahrani na Complex (2001)
Twenzetu - Chegge, Ferouz na Mh Temba (2005)
Elimu Mitaani.com - Dknob (2003)
Kitu Gani - Dknob (2007)
Tamara + ni wewe - Hard Mad
Eno maiki - Ziggy Dee (Uganda)
Nakupenda Mpenzi - Dudu Baya
get down - Prezo ft Naziz (Kenya)
Twenzetu - Chege
Baby Gal + wange - Mad Ice
Maria Salome - Saida Karoli
Kamanda + barua - Daz Nundaz
wanoknok + Taswira + dingi - Mandojo na domokaya
Picco - Kikongwe
Kwenye Chati - Balozi
Mtoto wa geti kali - Inspector Haroun
Elimu mtaani + sauti ya gharama - D knob
Mkiwa - K sal ft Ferooz
Salome + Julieta + Hi - Dully Sykes
Raha tu - AY
Mambo vipi - Mchizi Mox
Solid Ground Family - Bush party