TBT: Mwaka 1985 Scotland Yard walikuja Tanzania kuchunguza BOT na 1990 walikuja Kenya kifo cha Waziri Dr Robert Ouko

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Tujikumbushe matukio muhimu yaliyotokea hapo awali ktk nchu yetu na majirani zetu Pia.

Pamoja na mambo mengi yanayozungumzwa kuhusu msala huu wa Utekaji, utesaji, upoteaji na mauwaji ya Raia ambayo yameshika kasi ktk nyakati hizi ni wazi sasa tunaweza kuswma yafuatayo.

1. Mh Rais Amiri Jeshi Mkuu amethibitisha mpaka sasa hajawajua wanaohusika na matuko labda mpaka uchunguzi ufanyike na apewe ripoti kama alivyoagiza.
2. Mahakama haiwajui wahusika
3. Bunge haliwajui wahusika.
4. Jeshi la Polisi Tanzania bado haliwajuia wahusika.
5. Vyombo vingine vya ulinzi na usalama pia haviwajui wahusika.
6. Wananchi nao kwa wingi wao 60M hakuna anyewajua hao watekaji na wauwaji hivyo hofu imetanda kila mahali.
Kwa kusema hivyo ndio maana tunasema tunahitaji vyombo vyenye uwezo mkubwa na uzoefu na uaminifu usio na chembe ya shaka kutusaidia kuchunguza zahama hii inatotukabili kama Taifa.

Katika orodha ya Sheria zetu za Nchi hakuna mahali Sheria wala kanuni inazuia Kuomba vyombo au kushirikiana na vyombo vingine vya kimataifa kufanya uchunguzi kwenye uharifu ndani ya Nchi.

Kwani haitakuwa mara ya kwanza kufanya hivyo na pengine inaweza kuzidisha mahusiano na kujange uwezo kwenye vyombo vya ndani kiutalamu na uchunguzi.

Mwaka 1984 muda wa asubuhi Jengo la BOT pale ufukweni Dar es salaam llilishuhudiwa na maelfu ya watu likiteketea kwa moto, vyombo vya ulinzi na usalama viliorganize na kuhakikisha usalam na ulinzi mkali unawekwa ili kuhakikisha hakuna uharibifu unajitokeza wakati wa janga. Hata hivyo chanzo cha moto na madhara yake hayakufahamika mpaka Pale Serikali ililazimika kuomba msaada kwa Jeshi la Polisi la Uingereza, Scotland Yard.

Scotland Yard ni Kitengo Mahususi cha Jeshi la Polisi la Uingereza kilichobobea kwenye maswala ya kiuchunguzi ya uharifu wa kimataifa( internationa Organize crime Investigation section). Kinafahamika kama kikosi imara duniani kote kwenye maswala ya forensiki.

Pia wakati wa Utawala wa Daniel Arap Moi, Rais Wa pili wa kenya kilitokea kifo baada ya mauwaji ya Waziri wake wa Mambo ya Nje Dr Robert Ouko. Serikali ya Kenya ilikazimu kuwaita Team ya Scotland yard ikiongozwa na Kachero, Detective Super Intendent John Troon na wenzake wawili February 1990.

Kifo cha Dr Robert Ouko kilitokea miaka michache baada ya kupata misuko suko kutokana na hulka yake ya kukosoa utawala wa Kidikiteta wa Rais Moi ambapo kabla ya kifo chake alifunguliwa mashtaka mahakamani na akaamua Kujiuzulu baada ya kesi kuisha kati ya mwaka 1982 na 1985.

Report ya Uchunguzi ya Kifo cha Robert Ouko iliwekwa wazi na Wakenya wote wanapata fursa ya kuisoma na kuujua ukweli wa kile kilichojiri.

Soma Pia: Freeman Mbowe: Scotland Yard ya Uingereza ichunguze Matukio ya Utekaji na Uuaji nchini

Hivyo hatuna sababu ya kusua sua kufanya haraka kama kweli tuna nia ya dhati ya kukomesha matukio haya.
 
Tujikumbushe matukio muhimu yaliyotokea hapo awali ktk nchu yetu na majirani zetu Pia.

Pamoja na mambo mengi yanayozungumzwa kuhusu msala huu wa Utekaji, utesaji, upoteaji na mauwaji ya Raia ambayo yameshika kasi ktk nyakati hizi ni wazi sasa tunaweza kuswma yafuatayo.

1. Mh Rais Amiri Jeshi Mkuu amethibitisha mpaka sasa hajawajua wanaohusika na matuko labda mpaka uchunguzi ufanyike na apewe ripoti kama alivyoagiza.
2. Mahakama haiwajui wahusika
3. Bunge haliwajui wahusika.
4. Jeshi la Polisi Tanzania bado haliwajuia wahusika.
5. Vyombo vingine vya ulinzi na usalama pia haviwajui wahusika.
6. Wananchi nao kwa wingi wao 60M hakuna anyewajua hao watekaji na wauwaji hivyo hofu imetanda kila mahali.
Kwa kusema hivyo ndio maana tunasema tunahitaji vyombo vyenye uwezo mkubwa na uzoefu na uaminifu usio na chembe ya shaka kutusaidia kuchunguza zahama hii inatotukabili kama Taifa.

Ktk orodha ya Sheria zetu za Nchi hakuna mahali Sheria wala kanuni inazuia Kuomba vyombo au kushirikiana na vyombo vingine vya kimataifa kufanya uchunguzi kwenye uharifu ndani ya Nchi.

Kwani haitakuwa mara ya kwanza kufanya hivyo na pengine inaweza kuzidisha mahusiano na kujange uwezo kwenye vyombo vya ndani kiutalamu na uchunguzi.

Mwaka 1984 muda wa asubuhi Jengo la BOT pale ufukweni Dar es salaam llilishuhudiwa na maelfu ya watu likiteketea kwa moto, vyombo vya ulinzi na usalama viliorganize na kuhakikisha usalam na ulinzi mkali unawekwa ili kuhakikisha hakuna uharibifu unajitokeza wakati wa janga. Hata hivyo chanzo cha moto na madhara yake hayakufahamika mpaka Pale Serikali ililazimika kuomba msaada kwa Jeshi la Polisi la Uingereza, Scotland Yard.

Scotland Yard ni Kitengo Mahususi cha Jeshi la Polisi la Uingereza kilichobobea kwenye maswala ya kiuchunguzi ya uharifu wa kimataifa( internationa Organize crime Investigation section). Kinafahamika kama kikosi imara duniani kote kwenye maswala ya forensiki.

Pia wakati wa Utawala wa Daniel Arap Moi, Rais Wa pili wa kenya kilitokea kifo baada ya mauwaji ya Waziri wake wa Mambo ya Nje Dr Robert Ouko. Serikali ya Kenya ilikazimu kuwaita Team ya Scotland yard ikiongozwa na Kachero, Detective Super Intendent John Troon na wenzake wawili February 1990.
Kifo cha Dr Robert Ouko kilitokea miaka michache baada ya kupata misuko suko kutokana na hulka yake ya kukosoa utawala wa Kidikiteta wa Rais Moi ambapo kabla ya kifo chake alifunguliwa mashtaka mahakamani na akaamua Kujiuzulu baada ya kesi kuisha kati ya mwaka 1982 na 1985.

Report ya Uchunguzi ya Kifo cha Robert Ouko iliwekwa wazi na Wakenya wote wanapata fursa ya kuisoma na kuujua ukweli wa kile kilichojiri.

Hivyo hatuna sababu ya kusua sua kufanya haraka kama kweli tuna nia ya dhati ya kukomesha matukio haya.
Hakuna haja ya kuunda matume tume kila siku ni kupoteza muda na mali wakati tunajua cha kufanya.
 
Kama ni serikali ipendayo haki na kweli,muda ni huu.Sijajua kigugumizi kinatokea wapi.Au bado ni yaleyale kwamba hakuna wa kuwaelekeza cha kufanya?Ni kujitengenezea mwisho wenye sonona na upweke tu.
 
1. Mh Rais Amiri Jeshi Mkuu amethibitisha mpaka sasa hajawajua wanaohusika na matuko labda mpaka uchunguzi ufanyike na apewe ripoti kama alivyoagiza.

4. Jeshi la Polisi Tanzania bado haliwajuia wahusika.
5. Vyombo vingine vya ulinzi na usalama pia haviwajui wahusika.
Siyo kweli mleta mada. Kwa lugha ya kiburi na dharau aliyoitumia Samia juzi ni dhahiri kuwa anajua kila kitu na mauaji hayo yalifanywa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa maagizo yake.
 
Bado uchunguzi haujafanyika na Rais Mwenyewe atapewa majibu kama alivyoagiza. Lakini ikiwa kuna shida ndio maana tunahimiza vyombo mashuhuri vya uhakika vije visaidiane na vyombo vya ndani. Nina wasi wasi huenda kuna magaidi wameingia.
 
hakuna mahali Sheria wala kanuni inazuia Kuomba vyombo au kushirikiana na vyombo vingine vya kimataifa kufanya uchunguzi kwenye uharifu ndani ya Nchi.
Ni kweli, lakini si baada ya kujiridhisha kwamba vyombo vyombo vyetu havina uwezo wa kuchunguza? Hii ni hatua ya awali. Tuwe na subira.
Hata hivyo chanzo cha moto na madhara yake hayakufahamika mpaka Pale Serikali ililazimika kuomba msaada kwa Jeshi la Polisi la Uingereza, Scotland Yard.
Hile ripoti ilitolewa na watu wakaiona? Ilisemaje?

NB: Naunga mkono kuomba msaada ikiwa nchi haina uwezo, ila hii isifanywe kwa maneno ya mitaani. Ni lazima tuende kitaalamu.
 
Ni kweli, lakini si baada ya kujiridhisha kwamba vyombo vyombo vyetu havina uwezo wa kuchunguza? Hii ni hatua ya awali. Tuwe na subira.
Hile ripoti ilitolewa na watu wakaiona? Ilisemaje?

NB: Naunga mkono kuomba msaada ikiwa nchi haina uwezo, ila hii isifanywe kwa maneno ya mitaani. Ni lazima tuende kitaalamu.
Sahihi
 
Hile ripoti ilitolewa na watu wakaiona? Ilisemaje?
Waliomuua walitengeneza mazingira ya kuonesha kwamba amejiua kwa kujipiga risasi na kujichoma moto kwa kutumia disel.
Uchunguzi ulionesha alichomwa moto baada ya kumuua. Na kwamba walimvunja mguu na mokono kabla hajafa na pia walimpiga risasi tofauti na zile zilizokutwa kwenye magazini ya siraha yake pembeni mwa maiti.

Hata hivyo shuhuda na ushahidi mwingine ulibainisha aliuawa ktk viunga vya nyumba nyeupe ya Arap Moi.
 
Mleta mada unachanganya Swala la BoT Scotland Yard walikuja tu kuangalia tu pesa zao za pound za uingereza kama ziko salama hawakuja kuangalia mambo mengine hayo mengine waliachia vyombo vya usalama vya ndani ndio maana ripoti yao haikuwekwa hadharani waliwapelekea wenye pesa zao za pound

Jeshi la polisi halijashindwa kuwatambua ndio kwanza limeanza uchunguzi huwezi sema wameshindwa kuwapata bila kuwapa nafasi ya kuchunguza

Uchunguzi umeanza
 
Asante kwa kuchangia mada.

Kuhusu polisi wetu kuanza uchunguzi je hili ni tukio kwanza? Si la jana wala leo wala mwaka jana wala mwaka juzi.

Tukubali tusaidiwe na pia tupate uzoefu kwa wenzetu
 
Waliomuua walitengeneza mazingira ya kuonesha kwamba amejiua kwa kujipiga risasi na kujichoma moto kwa kutumia disel.
Uchunguzi ulionesha alichomwa moto baada ya kumuua. Na kwamba walimvunja mguu na mokono kabla hajafa na pia walimpiga risasi tofauti na zile zilizokutwa kwenye magazini ya siraha yake pembeni mwa maiti.

Hata hivyo shuhuda na ushahidi mwingine ulibainisha aliuawa ktk viunga vya nyumba nyeupe ya Arap Moi.
Mkuu; Mimi Quotation yangu ya moto ni kuhusu BOT kama ulivyoandika. Ndio nikaulzia ripoti ya Scotlandyard. Hebu ipitie vzuri halafu nasubiri jibu
 
Asante kwa kuchangia mada.

Kuhusu polisi wetu kuanza uchunguzi je hili ni tukio kwanza? Si la jana wala leo wala mwaka jana wala mwaka juzi.

Tukubali tusaidiwe na pia tupate uzoefu kwa wenzetu
Matukio ya utekaji yapo mengi na mengine wahusika mbona walidakwa vizuri tu mfano wa karibuni ni mtoto Albino aliyetekwa na kuuawa kule Geita watekaji na wauaji akiwemo padri na baba mzazi wa mtoto walidakwa

Pia kuna mfanyakazi wa mgodi wa Geita aliuawa na wasiojulikana mbons walidakwa wote na kuhukumiwa kunyongwa

Kesi ingine ya mfanyabiashara huko Songea kutekwa na kuporwa pesa na kuuawa na kutupwa porini mbona wahusika walidakwa na polisi Dodoma na wako mikononi mwao
 
Back
Top Bottom