Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Kati ya mwaka 1960 hadi 1966, Ufaransa ilifanya majaribio ya mabomu ya Nyuklia nchini Algeria katika maeneo mbalimbali ya jangwa la Sahara. Ufaransa ilifanya majaribio haya kwenye maeneo ambayo "walikodishwa" na Algeria kupitia mikataba iliyosainiwa kati ya Algeria na Ufaransa Ili kusitisha vita vya uhuru wa Algeria vilivyoua zaidi ya raia milioni 2 wa Algeria.
Ingawa makubaliano hayo hayakuhusu Ufaransa kutumia ardhi ya Algeria kama sehemu ya majaribio ya mabomu ya Nyuklia, Rais wa Ufaransa wa wakati huo Charles de Gaulle aliona ana haki ya kufanya chochote kwenye ardhi hiyo" iliyokodishwa".
Majaribio hayo yalihusisha majaribio ya chini ya ardhi ( underground) pamoja na majaribio ya hewani( atmospheric). Mojawapo ya mabomu yaliyotumika yalikuwa na nguvu mara nne ya bomu lililodondoshwa jijini Hiroshima.
Majaribio ya mabomu hayo ya Nyuklia yalisababisha madhara mbalimbali kwa raia wa Algeria kama vile vifo, saratani, kuzaliwa kwa watoto wenye ulemavu, upofu na magonjwa mengine.
Pia mionzi ya sumu iliyotokana na mabomu hayo ilisambaa nje ya Algeria hadi nchini Sudan pamoja na nchi nyingine za Afrika magharibi.
Kwa miaka mingi Ufaransa iliwaficha wakazi walioathiriwa na majaribio hayo hali iliyowafanya wasijue chanzo cha matatizo ya kiafya yaliyowapata . Vilevile nyaraka zilizohusu mahali palipotumika kwa ajili ya majaribio zilifichwa. Pia waathirika wa majaribio hayo hawakulipwa fidia.
Mnamo mwaka 2001 , Ufaransa ilianza mchakato wa kulipa fidia kwa waathirika wa majaribio hayo ingawa vigezo vilivyowekwa na Ufaransa vilisababisha waathirika wengi wakose sifa za kulipwa fidia.
Hadi leo kuna taarifa za siri kuhusu majaribio hayo ambazo Ufaransa imegoma kuzitoa.
Vyanzo:
"The Legacy of French Nuclear Testing in Algeria Shows How Nuclear Weapons Perpetuate Colonialism | Global Zero" The Legacy of French Nuclear Testing in Algeria Shows How Nuclear Weapons Perpetuate Colonialism | Global Zero
"France-Algeria relations: The lingering fallout from nuclear tests in the Sahara" France-Algeria relations: The lingering fallout from nuclear tests in the Sahara