Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,319
Mbeya/Zanzibar.
Kocha mkuu wa Yanga, Hans Pluijm amesema hana wasiwasi na mfumo wa 3-5-2 unaotumiwa na Azam FC tayari ameshapata mbinu ya kuwamaliza katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili akiwa kambini Mbeya, Pluijm anayependa kutumia mifumo ya 4-4-2 na 4-3-3, alisema licha ya fomesheni hiyo ya Azam kupata umaarufu katika Kombe la Kagame kwa kumaliza mashindano hayo bila kufungwa bao lolote, lakini akasema inaweza kufungika.
"Sitaweza kubadilisha fomesheni yangu, hii Azam inafungika kwa sababu wao watakuwa na mabeki watatu nyuma, wakati mimi nitakuwa nao wanne," alisema Pluijm.
"Nitatumia za kawaida na siyo vingine, kama unakumbuka mechi iliyopita na Azam tuliwamudu, lakini mwisho wa siku penalti ndiyo zilituondoa."
Akizungumzia namna atakavyoimudu Azam, Pluijm alisema: "Wao wanawategemea zaidi wale wachezaji watano wa kati, wakati mabeki wa pembeni ndiyo wanakuwa na majukumu mengi zaidi, kama utamzuia Kapombe (Shomari) pembeni ambaye ndiye anayepandisha kwa wingi mashambulizi mbele na mwepesi kwenye kukaba au mwenzake wa kushoto, Azam hawezi kufanya kitu."
Pia, Mdachi huyo alisema anaamini mchezo huo utakuwa mgumu na hasa kucheza na aina ya mchezaji kama Kipre Tchetche mwenye akili ya mchezo, nguvu na uamuzi wa haraka.
"Unajua mechi ni mechi, Azam ni timu nzuri na inahitaji uangalizi wa juu kucheza na timu yenye mshambuliaji kama Tchetche mwenye ana akili sana uwanjani ni mchezaji hatari kwenye kikosi cha Azam.
"Lakini kutokana na namna tulivyojiandaa na wachezaji wangu wakacheza kwa kufuata maelekezo tuliyofundishana, hakuna atakayetamba, najua ni namna gani tutakavyomdhiti huyo Tchetche na wenzake," alisema Pluijm kwa kujiamini.
Kocha wa Azam, Stewart Hall alisema kwa sasa hana uhakika na mfumo gani atautumia katika mchezo huo, alisema inategemea aina ya wachezaji watakaochaguliwa kucheza katika mechi hiyo.
Alisema mfumo wa 3-5-2 ambao ndiyo anaoutumia kwa sasa bado una nafasi katika mechi hiyo, lakini mabadiliko yanaweza kutokea kulingana na uchaguzi wa wachezaji wake.
"Wachezaji ndiyo wamekuwa wakitengeneza mfumo, Yanga ni timu kama zilivyo nyingine hatuwezi kubadilisha mambo mengi katika timu yetu kwa ajili ya mechi moja, tutaamua tutumie mfumo upi kulingana na wachezaji nitakaoamua kuwatumia," alisema Hall.
Chanzo: Mwananchi