TCHOUKBALL TANZANIA: Kwa mara ya kwanza tchoukball yaingia Tanzania

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
Habarini ndugu zangu na ashukuriwe mungu kwa afya alotujalia na uzima tele. Ni matumaini yangu nyote humu ni wazima. Tanzania ni moja kati ya nchi duniani zinazothamini michezo huku michezo mingi ikiwa inafahamika hapa nchini. Licha ya yote, kwa muda mrefu mchezo wa tchoukball ulikuwa haufahamiki nchini Tanzania hadi ulivyoingia hivi majuzi na vijana kadhaa kupata mafunzo yake mafupi huko mkoani Arusha.

Japo ni mchezo mpya hapa Tanzania lakini wenzetu wa Kenya na Uganda walishatutangulia katika mchezo huu na tayari Uganda walishatayarisha mashindano yake.

Ni mchezo usiotumia nguvu nyingi sana kama michezo mingine bali huu ni mchezo wa kutumia nguvu kidogo akili nyingi. Ni mchezo unaojulikana pia kama peace game kwani siyo mchezo wa kukabana kama mpira wa miguu. Ni mchezo unaochezwa na watu wa jinsi zote, wakubwa kwa wadogo.

Tutaendelea kuhabarishana kuhusu mchezo huu,

Asante..
 
sijawahi uhusikia. unachezwaje na kwa staili ipi
 
sijawahi uhusikia. unachezwaje na kwa staili ipi

mchezo huu unafanana kana handball japokuwa siyo handball,nikiwa na maana kuwa unachezwa na mikono na hairuhusiwi kukaba ili inatuhusiwa kudeffense goli. magoli yapo mawili na mchezaji anaruhusiwa kufunga upande wowote. mchezo huu unachezwa na watu saba kila timu,jumla kumi na nne.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…