TCRA - 2024: Idadi ya Utumiaji wa Intaneti umefikia Milioni 48. Vodacom inaongoza utoaji intaneti kwa njia ya simu, TTCL ikiburuza mkia

TCRA - 2024: Idadi ya Utumiaji wa Intaneti umefikia Milioni 48. Vodacom inaongoza utoaji intaneti kwa njia ya simu, TTCL ikiburuza mkia

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Kwa mujibu wa ripoti ya Takwimu za Mawasiliano ya TCRA iliyotoka Desemba 20204, inaonesha kuwa idadi ya utumiaji wa Intaneti imeongezeka kwa 16% kutoka milioni 41.4 kwa robo ya mwaka iliyoishia Septemba 2024 hadi milioni 48 kwa robo ya mwaka iliyoishia Disemba 2024.

Huduma ya intaneti inatolewa kwa kutumia laini za simu, waya (faiba), na mawimbi (wireless). Idadi ya utumiaji wa intaneti inatokana na laini/waya ambazo zimetumia huduma ya Intaneti angalau mara moja katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, bila kujali teknolojia iliyotumika (FTTX, 2G - GPRS na EDGE, 3G, 4G, au 5G).
Screenshot 2025-02-06 at 13.16.56.png

Aidha, Mgawanyo wa huduma ya Intaneti kwa njia ya simu kwa kila mtoa huduma kwa robo mwaka inayoishia Disemba 2024 inaonesha kuwa Vodacom inaongoza kwa kutoa Intaneti kwa asilimia 34, ikifuatiwa na Yas kwa asilimia 30 huku TTCL ikiwa ya mwisho kwa asilimia 3.
Screenshot 2025-02-06 at 13.18.39.png

Pia soma: KERO - TTCL ni sikio la kufa! Haiwezekani kwa zaidi ya miezi sita nimeomba huduma ya fiber nyumbani wananizungusha tu

Katika hatua nyingine, ni kuwa Intaneti ya kasi kwa huduma ya simu ndiyo njia inayopendelewa zaidi kupata Intaneti, ikiwa na laini 25,598,698. Teknolojia ya 2G bado ina matumizi makubwa, ikiwa na laini 22,250,574. Teknolojia za Faiba Nyumbani (Fiber to the Home - FTTH) na Faiba Ofisini (Fiber to the Office - FTTO) zina idadi ndogo ya laini 71,661 na 11,540 mtawalia.
Screenshot 2025-02-06 at 13.39.41.png

Matumizi ya huduma ya Intaneti huhesabiwa kama kiasi cha data (katika Petabytes) kilichotumiwa katika kipindi husika. (1 Petabyte = 1000³ Megabytes).

Jedwali 1.9.2 linaonesha kuwa kila usajili wa intaneti ulitumia wastani wa GB 4.49 kwa mwezi Disemba ambayo ni zaidi ikilinganishwa na Oktoba na Novemba.

Screenshot 2025-02-06 at 13.41.56.png
 
Back
Top Bottom