TCRA: 80% ya tamthilia zinazorushwa kwenye TV ni za nje

TCRA: 80% ya tamthilia zinazorushwa kwenye TV ni za nje

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevihimiza vyombo vya habari kuangalia uwezekano wa kutoa nafasi kwa tamthiliya, muziki na michezo zenye maudhui ya ndani ili kulinda utamaduni na nembo ya Taifa.

Akizungumza kwenye mkutano wa wadau mbalimbali wa vyombo vya habari, sanaa na michezo mwakilishi wa TCRA, Andrew Kisaka alisema tafiti zinaonesha asilimia 80 ya tamthiliya zinazorushwa ni za nje.

Aidha, alisema angalau muziki unaopigwa kwa asilimia 80 umebeba maudhui ya ndani isipokuwa kuna changamoto kwenye ujumbe ulioko ndani yake nyingi zinazungumzia mapenzi kiasi kwamba hakuna kitu ambacho mtu anaweza kujifunza.

“Licha ya kwamba kuna baadhi ya vyombo vya habari vimeanzisha chaneli maalumu kuonesha filamu na tamthiliya za ndani bado hazipewi nafasi kubwa/hazikuzwi sana kama ilivyo kwa zile za nje,” alisema.

Alisema afadhali michezo ya ndani imekuwa na kupewa nafasi tofauti na miaka ya nyuma ambapo kwa sasa mitaani imekuwa ikijadiliwa kila mahali huku akisema kwenye picha jongefu asilimia 80 ni za nje ya nchi, katuni za watoto asilimia 95 ni za nje akihimiza umuhimu wa kutengeneza zenye maudhui yanayoendana na utamaduni wa nchi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Habi Gunze alisema sababu ya kuandaa semina hiyo ni baada ya kugundua kuna malalamiko kutoka kwa watumiaji wa vyombo vya habari wakisema tamthiliya zinazorushwa nyingi ni za nje na kutaka itafutwe suluhisho kutoka kwa wadau hao.

Mkurugenzi wa Plus Tv, Ramadhan Bukini alisema changamoto iliyopo maudhui ya vipindi vya ndani kwa mfano ngoma za asili na vingine wanashindwa kurusha kwa sababu picha wanazopokea hazina viwango na ubora utakaovutia huku mdau mwingine kutoka Chanel ten, Albert Kilala akisema kuna gharama za kutengeneza maudhui ya ndani akitaja fedha, rasilimali watu na vifaa kwa ajili ya kuandaa vitu vizuri kwani kunahitajika uwekezaji mkubwa.
 
Tatizo ni za hapa Bongo kukosa;
ubunifu
mvuto
hazina mafundisho zaidi ya ngono zao!
 
Nyie watu mnapenda kujichosha Sana...huku kwenye DStv hatuhitaji huo ujinga wenu pelekeni azam na kwingineko,naachaje kuangalia NAT GEO WILD alafu niangalie SAFARI CHANNEL au naacha vipi kuangalia Mnet movies alafu niangalie bongo movies?
 
Nyie watu mnapenda kujichosha Sana...huku kwenye DStv hatuhitaji huo ujinga wenu pelekeni azam na kwingineko,naachaje kuangalia NAT GEO WILD alafu niangalie SAFARI CHANNEL au naacha vipi kuangalia Mnet movies alafu niangalie bongo movies?
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji2772]

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
Hakika, ila wakijitahidi kufanya hivyo mnawafungia...
 
Back
Top Bottom