TCRA: Akaunti za Pesa Mtandao zafikia milioni 63.2. Miamala 3,737,202,434 yafanyika kwa mwaka 2024

TCRA: Akaunti za Pesa Mtandao zafikia milioni 63.2. Miamala 3,737,202,434 yafanyika kwa mwaka 2024

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Kwa mujibu wa Ripoti ya Takwimu za Mawasiliano iliyotolewa na TCRA, Desemba 2024, idadi ya akaunti za pesa mtandao ambazo zilitumika angalau mara moja katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita iliongezeka kutoka akaunti milioni 60.8 katika robo ya mwaka iliyoishia Septemba 2024 hadi milioni 63.2 katika robo ya mwaka iliyoishia Desemba 2024.
Screenshot 2025-02-07 at 13.21.11.png

Ripoti hiyo inaonesha kwa Vodacom imeongoza kwa usajili wa akaunti za pesa mtandao kwa miezi mitatu ya mwisho wa mwaka 2024, ikifuatiwa na Mixx by Yas, Airtel Money, kisha HaloPesa, T-Pesa ya TTCL na ya mwisho ikiwa AzamPesa. Jedwali linaonesha idadi ya akaunti kwa kila mwezi.
Screenshot 2025-02-07 at 13.24.51.png
Screenshot 2025-02-07 at 13.30.38.png

Aidha, Katika idadi ya miamala iliyofanyika katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho wa mwaka 2024, M-Pesa imeongoza kwa kuwa na miamala mingi ikifuatiwa na Airtel Money iliyokuwa ya tatu katika usajili wa akaunti za pesa mtandao kwa kipindi hicho.

Mixx by Yas imeshika nafasi ya 3 ikifuatiwa na HaloPesa huku Azam Pesa ikiipita T-pesa ya TTCL iliyoburuza mkia, na kushika nafasi ya 5. Idadi ya miamala kwa kila mwezi ni kama inavyoonekana.
Screenshot 2025-02-07 at 13.33.41.png

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita idadi ya miamala ya simu ilikuwa kubwa katika mwaka 2023 huku ikiwa ndogo mwaka 2020​

Screenshot 2025-02-07 at 13.38.28.png

 
Back
Top Bottom