Elections 2010 TCRA disassociates itself with defamatory messages against Slaa

Bado naendelea kuchunguza iwapo IMSI inaweza kuwa stored manually kwenye database ya Home Location Register (HLR) na kubypass automatic storage. Ufumbuzi wa hili unaweza kuamua iwapo HLR Lookup ina maana yoyote hapa au kuna watu ndani ya local operators wetu wanachezea database. Nitarudi baadaye.
 
Kwa nini asiulizwe balozi wa Finland??
 
Shimbo yupi bana? Kama ni huyu mjeshi hujui kwamba naye ni mwanakamati kwenye vikao vilivyotafuta namna ya kuwahofisha raia. Tangu lini nyani akamkemea tumbili kuhusu ulaji mahindi mabichi.
.
 
TISS na TCRA si ndio haohao, nafikiri kuna sababu pia ya kuususia mtandao wa vodacom, uchafu wanaoufanya unahatarisha amani na demokrasia nchini

mpendwa sio vodacom pekee....mi kwangu imeingia kwenye zain...cha kufanya kwa sisi sote tulioipata hii msg tuanze kufanya mawasiliano na ndugu zetu wale ambao tunahisi wataogopa kwa vitisho vya namna hii na kubadilisha mawazo ifikapo Oct 31.....tuwaelimishe na kuwasisitiza wampigie nani kura siku hiyo kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu
 
Wakuu,

Kuhusu hii SMS ya Finland ambayo inasema, "Slaa ni mropokaji na mgomvi anatukana vyombo vya ulinzi na usalama. Anataka damu imwagike ili mradi aingie Ikulu. Tumkatalie kuigeuza nchi yetu Somalia."

Nimeangalia michango ya wadau mbali mbali ila nikabaki na swali moja. Je kuna uwezekano kuwa Slaa anatuchezea?

Kwamba hii meseji inawezekana pia ikawa imetumwa na timu ya Slaa ili kujijengea mazingira ya u-victim (kuonewa) ili apate cha kuongea na kuamsha hisia za watu dhidi ya CCM kwa staili ya kinyume nyume (reverse psychology).

Au kuna ushahidi gani unaoonesha kuwa hii meseji imetengenezwa na watu wa CCM?
 
Nyie Chadema vipi mnalialia tu?

Si na nyie andikeni na kuzituma? Kuna uwezekano wa kuandikia kwenye computer na namba unafanya tu KUJARIBU. Ikikubali, sawa na ikikataa basi tena.............
 
Tatizo lako ni kuwa UNAANGALIA badala ya KUSOMA..............
 
Mungu akusamehe hujui unalosema wewe. Anyway kila mtu na mawazo yake.
 
Sidhani kama hili linamhusu shimbo. Jf sasa inageuzwa kuwa eneo la kufanya siasa za majitaka
 
Mimi sijawai pewa izo vocha ila CCM wanatuma msg zao namba yangu wameitoa wapi?
Jamani hii message imekaa kichochezi sana ndo maana watu wanalalamika kama Shimbo angekuwa serious ilibdi waanze na aliyetuma hii msg bse ni ya kichochezi kuifananisha Tz na kwa Akina Kinana ooh sorry Somalia si kutishia raia wasimchague Dr
 
Ingekuwa hiyo namba ina code ya Tanzania angalau ingekuwa na impact. Wamenitumia Jana na leo asubuhi. Wamechemsha kwani nilishafanya uchaguzi. Hata mimi niko tayari kumwaga damu kuliko kuendelea kuishi kwa tabu.
 
Mi naona hao ndio wanaohatarisha usalama wa nchi
 
Sidhani kama hili linamhusu shimbo. Jf sasa inageuzwa kuwa eneo la kufanya siasa za majitaka

Shimbo alitoa onyo la hofu kwa wananchi bila ku ainisha watu au kikundi cha watu kinachotishia amani ya nchi. Alipopewa changamoto ya kuwafikisha mbele ya sheria watu hao ambao aliwatuhumu bila kuwataja alikaa kimya kama paka aliyemwagiwa maji baridi. Sasa kuna ushaidi wa uhakika wa watu wanaotembeza ujumbe wa SMS kwa makusudi ya kuharibu amani. Hapaswi kukaa kimya.
 
Is it possible that the network provider's main frames have been hacked?nalo linawezekana..
 
Ah! tsy! Acheni kulialia bana! Hii ni vita tumia silaha yoyote unayohisi itamzoofisha adui, kumbe hamkuijua ngoma mnayo icheza enh? Muulizeni Lipumba 2005. Yaani Dk Slaa hajapigwa hata kirungu kimoja tayari mnachanganyikiwa na kupoteza dira, kuleta mabadiliko sio mchezo,ACHENI KULIA LIAtafuteni silaha ya kujibu mapigo na kumrudisha nyuma Adui. Ushindi ni ushindi tu haijalishi umepatikana vipi.
 
Wakuu Tusikurupuke kushutumu, hivi ukipata msg ya kukutukana,kukukashifiwa au kutishiwa kuuawa utaenda kushtaki TCRA au Polisi? obvious the chain of command katika masuala hayo itaanzia polisi.

Tofautisha ujumbe unaotukanwa na mtu mmoja,na unakujia wewe tu na si kila mtu,halafu pia utofautishe kuwa ujumbe huu umekuja kwenye kipindi cha kampeni.Lengo kuu la ujumbe huu ni kumpaka matope Slaa kwa wapiga kura,....kuripoti police ni utaaratibu,lakini wenye uwezo wa kufuatilia chanzo cha ujumbe huo ni TCRA.Halafu jambo jingine mbona hatujasikia makampuni ya simu yakilalamika kuwa mitambo yao imekuwa hacked,ndo maana hao wahuni wana broadcast kwa wateja wao?au nao ni sehemu ya njama hizo,au nao wanasubiri malalamiko ya wateja wao?
Nawatahadharisha CCM,ingawa najua kuwa hamtatilia maanani,Tanzania haina tofauti na nchi zingine ambazo ziliingia kwenye machafuko kwa sababu ya kuchoshwa na vitendo vya uporwaji wa haki zao wa wazi wazi.Mkijifanya kuwa mmeziba masikio na mnalotaka na liwe basi historia itawahukumu,Mungu yupo muamini msiamini na anasikia vilio vya watu.Ipo siku ,mtayajutia mnayoyafanya leo na itakuwa majuto ni mjukuu.
 

Mtoto wa fisadi
 
CCM wameshachanganyikiwa mwaka huu.

Niko kwenye IT/Telecommunication Industry for quite sometime now.

TCRA hawawezi kutudanganya kwamba hawawezi kuijua namba hiyo nani kaipiga. Zoezi la uhakiki wa namba zote za Wa-tz walishalifanya. Hiyo namba inaonekana ni International(yaani nje ya nchi yetu). Mitambo yote ya Simu whether Mobile au Fixed ina mifumo ya MALICIOUS TRACE CALL. Mfumo huu unaweza kufuatilia na kubaini namba hii ilipigwa saa ngapi,wapi na nani aliyeipiga! Kwa hiyo TCRA wanaweza wakafuatilia kupitia makampuni ya simu na kuing'amua nani mwenye namba hiyo.

Kinachoonekana hapa ni kwamba CCM watakuwa wamewatumia makada wao walioko Finland kwenye Ubalozi au mtoto yeyote wa kigogo aliyeko huko kuandika hiyo sms ya kumchafua Dk. Slaa na kuituma kwenye baadhi ya namba za Watanzani hapa nchini ili kuwatia hofu.

Kila rika na zama zake.Propaganda za kudanganya watu na kuwafanya hamnazo umeshapita.
CCM tangazeni sera zenu mbovu zilizoshindikana badala ya kufanya Siasa za Maji taka. Ni ujuha huo.

Mbona mwaka huu mnalo babu. Maana mmeanzia kwenye NDOA YA DK.SLAA mkachemsha, mkaja kwenye KUTUMIA JWTZ bado mkachemha, mkaja kwenye MBINU ZA KUTUMIA utafiti wa ki-Profesa Maji marefu wa kina SYNOVATE NA REDET bado mnachemka. Mmekuja kwenye MPANGO WA KUCHAKACHUA MATOKEO bado watu wako ngangari. Sasa mmehamia kwenye SMS!! Kesho sijui mnakuja na mbinu gani.
Ama kweli mfa maji haaachi kutapatapa.

CCM KWISHINE,CCM BYE BYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!
 
Hivi haya matope wanataka kumpaka nani? Jukumu lao ni kuzuia namba kama hizi zenye kushusha hadhi ya jamii na kuhatarisha usalama wa taifa na wao wanapaswa kutoa taarifa polisi lakini yaeleka wanatutupia mzigo sisi. Hivi wanafikiri kazi yao ni kupokea mishahara tu?

Are they serious?


 
CCM ni mafisadi, kwanini watumie namba za nje/
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…