Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Tarehe 06/11/2019 nilisajiri laini yangu ya AIRTEL na kupewa namba ya usajiri, tarehe 19/07/2021 laini yangu ya AIRTEL ikafungwa kwa madai ya kutosajiriwa! Nikalazimika kwenda kwenye ofisi za AIRTEL na nilichoambiwa huko ni maluweluwe eti siku mbili zilizopita nilisajiri laini kwa alama za vidole!
Baada ya malumbano wakaifungua na kunipa namba mpya ya usajiri, jambo moja nililogundua ni sikuwa peke yangu niliyefungiwa bali walikuwepo wengine pia. Baada ya sakata langu mke wangu naye sasa amefungiwa laini yake ya AIRTEL naye imemlazimu aende kwenye ofisi ya AIRTEL na wamemahidi kuifungua baada ya saa 24!
TCRA ijue kuwa inapomfungia raia mwema bila sababu ni kwamba raia huyo anakosa mawasiliano muhimu na walengwa wake na pia anapoteza muda wa maongezi aliopewa na hafidiwi, hii ni dhuluma.