TCRA inawaendesha wamiliki wa mitandao ya simu kadri watakavyo

TCRA inawaendesha wamiliki wa mitandao ya simu kadri watakavyo

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Walianza na kusajili line kwa alama za vidole, wamiliki wa mitandao wakaishiwa nguvu wakijua kuwa sasa mavuno yatapungua kwakuwa watumiaji (walaji) watapungua.

Ashukuriwe Mungu watu wakawasajilia watu wao wa karibu maisha yakaanza kutengamaa.

Sasa TCRA inapofosi mtu awe na line moja tu kwa kila mtandao nadhani bado hawajajua kuwa sisi tuliwasajilia watu kwasababu kuu 2.

1. Kuna watu, vijana wadogo hawajafikia umri wa kupata kitambulisho cha uraia lakini wamepevuka na wanastahili kumiliki simu.

2.Kuna watu wetu wa karibu juhudi za kupata NIDA I'd ziligonga mwamba au hazijakamilika nao tuliwasajilia.

Kila mtu aliyempa line mwenzake basi amejiridhisha vya kutosha kuwa huyo mtu ni salama kwake na kwa taifa.

Kwa mwendo huu makampuni ya simu yatapoteza 15%_25% ya mapato yake soon endapo tu watalazimisha hili jambo la kumiliki single line kwa kila mtandao
 
Binafsi nimetamani sana kuelimishwa madhara ya kumiliki sim card mbili za mtandao mmoja. Maana nimeyatafakari, sijaweza kuyang'amua zaidi ya faida.

Nyumbani Nina simu ya nyumbani naitumia kuwasiliana na watoto na Dada Wa kazi nyumbani, just in case; Pia nina line nimeweka kwenye modem kwa ajili ya Internet kwenye PC Leo hii ninaambiwa kuwa nitahukumiwa kulipa faini Milioni Tano sababu Ninatumia sim card tofauti kwenye mtandao mmoja..

TCRA tuelewesheni RAIA tupate ufahamu, vitisho vya kutufunga na kutulipisha Faini siyo Mwafaka.
 
Wale matapeli ndio mwisho wao huo
 
Hiyo Ni Moja ya sheria mbovu kabisa zilizopitishwa na Bunge la Tanzania
Ilipitishwa na hili hili Bunge la yule anayepiga wenzako marungu ya kichwa!? Kama ni hivyo hiyo itakuwa amri ya yesu wa chattle.
 
Hivi eti ofisi za NIDA bado ziko wazi nataka kesho niende kukifuta kitambulisho changu
 
Nimeshachukua line yangu ya safaricom nasubiria kinuke nifanye yangu .. tena maeneo ya mipakani usipokua na line ya voda hii mitandao mingine inasoma 2G
 
Back
Top Bottom