TCRA kuanza ukaguzi wa Vifaa vya Mawasiliano ya Kielektroniki kwenye Nchi vinakoagizwa

TCRA kuanza ukaguzi wa Vifaa vya Mawasiliano ya Kielektroniki kwenye Nchi vinakoagizwa

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
4jiRxTMTQK7HQQExXmQmnG-1200-80.jpg

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), John Daffa amesema kuwa ukaguzi utaanza Mei 23, 2023 kwa lengo la kuepusha na kudhibiti uingizaji wa Vifaa vilivyokwisha muda wa matumizi Nchini.

TCRA imesema Hatua hiyo ni katika kutekeleza Kanuni zilizoazimiwa katika Mkutano wa Taasisi za Mawasiliano za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACO) zinazotaka vifaa vyote vilivyopita muda wa matumizi kupelekwa kwa watoa huduma wenye leseni za kukusanya, kukarabati au kuendesha mitambo ya kuvichakata.

Takwimu zinaonesha mwaka 1998, Tanzania ilikuwa na Tani 2000 za kiwango cha Taka za Kielektroniki, lakini hadi kufikia mwaka 2019 kiwango kiliongezeka hadi kufikia Tani 19,000 za ujazo.

================

Waagizaji wa vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki kutoka nchi mbalimbali kuja nchini wameelezwa kuwa kuanzia Mei 23 ya mwaka huu vifaa hivyo vitatakiwa kukaguliwa katika nchi vinapoagizwa ili kuepusha kuingiza vifaa vilivyokwisha muda wa matumizi.

Pia imewataka watengenezaji na waingizaji wa vifaa hivyo, kulipa ada ya usimamizi wa taka za kielektroniki kwa kila kifaa kinachoingizwa kama gharama za usimamizi wa vifaa hivyo vinapofika mwisho wa matumizi.

Hatua hiyo ni katika kutekeleza maazimio ya mkutano wa tano wa Taasisi za Mawasiliano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACO) kudhibiti ongezeko la taka za kielektroniki.

Takwimu zinaonyesha kwa Tanzania mwaka 1998 taka za kielektroniki zilikuwa tani 2,000 ila hadi kufikia mwaka 2019 taka hizo zilifika tani 19,000.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, John Daffa amesema kuwa utekelezaji wa utaratibu huo ni kwa mujibu wa kifungu 83(4) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Sura ya 306 kama ilivyoboreshwa Mwaka 2019)TCRA inajukumu la kusimamia vifaa vya mawasiliano ya kieletroniki pale vinapofika mwisho wa matumizi.

Amesema kanuni hizo zinataka kuhakikisha kuwa vifaa vyote vilivyofika mwisho wa matumizi vinapelekwa kwa watoa huduma wenye leseni za kukusanya, kukarabati au kuendesha mitambo ya kuchakatwa vifaa vya mawasiliano pale vinapofika mwisho wa matumizi.

"Katika utekelezaji wa jukumu hill TCRA imeingia kandarasi na Kampuni ya M/S BUREAU VERITASI TANZANIA LIMITED kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki kwenye nchi vinakoagizwa ili kuhakiki kuwa vifaa hivo havijafika mwisho wa matumizi pamoja na kuwezesha ukusanyaji wa ada za usimamizi wa taka za kielektroniki,"amesema.

Ameongeza kuwa kuanzia Mei 23 mwaka huu maombi yote ya kuingiza vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki yatawasilishwa kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya https://verigates.tcra- bureauveritas.co.tz ili kuwezesha uwasilishwaji wa taarifa zote za vifaa vinavyoagizwa.

"Baada ya maombi kupokelewa, uchambuzi tathmini kuhusiana na vifaa vinavyoagizwa pamoja na ada ya usimamizi wa taka za kielektroniki itafanyika ili kuruhusu hatua zinazofuata kutekelezwa," alisema.

Alifafanua kuwa uingizaji wa vifaa vya mawasiliano nchini unahitaji leseni tofauti yaani Importation License na vifaa vyote vitakavyoingizwa nchini vinatakiwa kuhakikiwa ili kutathmini ulinganifu na mwingiliano wakati wa matumizi.

Hata hivyo, alisema kuwa mtumiaji wa vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki hatahusika katika gharama hizo na kwamba hakutakuwa na ongezeko la gharama za ununuzi wa vifaa hivyo hapa nchini.

MWANANCHI
 
ulaji eti kutembelea nchi wanazotengeneza! Jabir naye kumbe mwizi! au dili la NAPE
 
Back
Top Bottom