TCRA mnahamasisha jamii kuchangamkia fursa za uchumi wa kidigiti wakati mnaongoza kukandamiza raia mtandaoni!

TCRA mnahamasisha jamii kuchangamkia fursa za uchumi wa kidigiti wakati mnaongoza kukandamiza raia mtandaoni!

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Wakuu,

Feb 6 Mkurugenzi Mkuu TCRA Dkt. Jabir Bakari alisema dhima ya serikali ni kuhakikisha jamii inanufaika kwenye uchumi wa kidigiti, uchumi ambao shughuli zote zinategemea TEHAMA, na kwamba ili tuweze kunufaika ni lazima tutengeneza jamii yenye fursa ya kutambua fursa zinazopatikana kwenye teknolojia. Hii ilikuwa katika mashindano ya fainali ya Cyber champions yaliyofanyika UDOM chini ya TCRA


Ni fursa gani mnataka jamii izichangamkie wakati kuna vikwazo kibao upande wa digitali? Ni Tanzania pekee ndio tunaconder chaneli za youtube kama TV🙄 mradi tu muwabane wanaogusa maslahi yenu. Namna hii mnategemea watu watachangamkia fursa na ubunifu kuongezeka?

Mtu kuwa na chaneli hiyo anatakiwa kulipiwa laki 5 sijui kila baada ya mwaka au miaka 3 (nimesahau kidogo hapa)! Hamnuoni mnazidi kuwakandamiza hawa mnaowaambia wachangamkie fursa?

Maslahi ya kiongozi/serikali/Rais yakiguswa tu mnakimbilia kufungia chombo, na hapo mnakuwa mnatumima haki yetu ya kupata taarifa. Hii ndio mnaita mazingira mazuri ya kumfanya mtanzania kuchangamkia fursa hizo?

Mnaanzisha mpaka kodi kwa content creators lakini hakuna mifumo mizuri ya kuchochea uchumi kidigitali, ni fursa zipi mnazotaka sisi wananchi tuchangamkie?

watengeneza maudhui mtandaoni tushapiga kelele wee kuhusu kupata mfumo wa malipo ili tuwe na vigezo tuanze kufaidia na maudhui yetu lakini kimya! Mtu kulipwa inabidi hadi abidili location yake. Ni fursa gani mnazotaka sisi wananchi tuzichangamkie?

Halafu, kwanini mmekimbia X? Mnachochea jamii kunufaika na uchumi wa kidigiti lakini nyinyi ndio wa kwanza kupinga vyombo hivi, na ni kwasababu gani? Serikali inakosolewa huko, kuna mtu kapigwa spana sababu ya kutowajibika!

Dunia inakimbia na kuchangamkia fursa lakini sisi tuko bize kukandamiza watu huku nje mnapiga kelele kana kwamba mnamaanisha.

Mkiendelea kulinda maslahi ya watu wachache tutaendelea kuona watanzania wakienda nchi nyingine na kuwekeza huko huku sapoti ya serikali ikibaki kuwa maneno kwenye kanga tu.

Fanyeni mnachohubiri, kama tunataka kweli Tanzania iendelee kidigitali mbadilike, serikali isimame kweli kwenye regulation sio kudhibiti kwa kuzuia na kuweka mazingira magumu nchini huku mkitegemea tupige hatua.
 
Back
Top Bottom