TCRA na Kampuni za Simu zirudishe vifurushi vya data za Wateja baada ya Mitandao kuzimwa

TCRA na Kampuni za Simu zirudishe vifurushi vya data za Wateja baada ya Mitandao kuzimwa

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Makampuni ya mawasiliano nchini yamezima data takriban wiki moja sasa. Wakati yakizima, hayakuwatangazia wateja juu ya uzimaji huo, na hivyo wateja wengi wakajikuta vifurushi walivyokuwa wameweka kwenda bure!

Lakini pia, kwa wale ambao hawakujua kuwa kuna kuzimwa kwa makusudi kwa mtandao waliendekea kununua vifurushi vingine wakidhani vifurushi vyao vya awali vimekwisha na hivyo kuingia hasara mara mbili, yaani kununua kifurushi usichokihitaji na pili kushindwa kukitumia kifurushi hicho.

Ninayataka Makampuni ya data Voda, TiGO, Airtel, Halotel na mengineyo yarudishe pesa zote za wateja za data walizozichukua huku wakijua hawawezi kutoa huduma ya internet kwa wateja.

Huu ni wizi, ni kunufaika kwa kupata pesa ambazo hukuzifanyia kazi. Ni uporaji wa fedha za wananchi.

Tunaitaka Serikali na TCRA ichukue jukumu la kuhakikisha wananchi wanakuwa compensated kwa Vifurushi vya data ambavyo hawakuvitumia mpaka muda ukaexpire.

Siyo wananchi wote walikuwa na VPN, wengine vifurushi vyao vilipotelea hewani, Tunataka kujua hizo pesa zimekwenda wapi na kwa nani.
 
Wameshazoea vya kunyonga hao.. Sina haja hata na hayo marudisho yao! Maana hawajui kusimamia kazi zao na hili la makampuni naona Kama wanaonewa tu mzizi ni huyo tcr nani sijui huko!.. badala aendeshe ye anaendeshwa!.. Ni aibu hata kujiita uchumi wa kati na wakati huohuo nyenzo Kama mawasiliano tena ya internet Ni yakusuasua!.. wao hawapo kwaajili ya kutatua changamoto bali kuongeza. Bora Elon musk arushe mi satellite huko tutumie hizo internet za wanaojua kuliko hizi za kishamba na masimango na waoga inakera tena inakera haswa!.
 
Washatuchukulia poa...Hili nalo litapita kimya kimya na maisha yataendelea.
Waafrika sisi ni wapole sana, wanyonge hadi kwenye haki zetu, tunachukuliwa poa na mamlaka kama shamba la bibi, hatujui hata yanayofanywa ni sawa au si sawa, ni kwa faida yetu au la,ni kwa makusudi au upendo! SISI NI BORA LIENDE, BORA LIPITE
 
Makampuni ya simu hayajazima data, wao wenyewe wanapata hasara vibaya mno.

Haya malalamiko yako yanawahusu TCRA ndiyo wamefanya huu utopolo.
Kwa sababu wao ndio wanapokea pesa, wao ndio wabanwe ili warudishe, kama na wao watawabana hiyo mamlaka ni juu yao.
 
Wameshazoea vya kunyonga hao.. Sina haja hata na hayo marudisho yao! Maana hawajui kusimamia kazi zao na hili la makampuni naona Kama wanaonewa tu mzizi ni huyo tcr nani sijui huko!.. badala aendeshe ye anaendeshwa!.. Ni aibu hata kujiita uchumi wa kati na wakati huohuo nyenzo Kama mawasiliano tena ya internet Ni yakusuasua!.. wao hawapo kwaajili ya kutatua changamoto bali kuongeza. Bora Elon musk arushe mi satellite huko tutumie hizo internet za wanaojua kuliko hizi za kishamba na masimango na waoga inakera tena inakera haswa!.
Mkuu inakera inakera tena sana, lakini wewe ungeweza kupinga agizo la mfalme Jiwe? Watz ni waoga sana na hawana ushirikiano hivyo inapelekea viongozi kishindwa kufanya maamuzi yaliyo sahihi kwa wananchi kwa maana yakimkuta anajikuta yuko peke yake .
 
Wazime pia umeme na jua ili tuome kama maandamano ya gizani yatawezekana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom