Sitegemei mamlaka husika zikae kimya juu ya hili,hii ni aibu haiwezekani ndani ya nchi yetu wenyewe, kodi zetu wenyewe na huduma zetu wenyewe zitutese kwa kukosa hudama za kimtandao! Wengi wanatumia VPN kuperuzi.
Kwanini jambo hili lijitokeze wakati huu wa uchaguzi ambapo ilitakiwa mawasiliano yaimalike zaidi lkn imekuwa kinyume chake! Bila kuangalia imeathiri biashara za watu! Kuna watu wamekula hasara ni aibu hii kwa taifa maana inaonyesha ipo namna tena inatia shaka!.
Si ombi bali ni lazima vyombo husika vije vijibu nini kimetokea? Kwanini? Na kwanini iwe wakati huu wa uchaguzi?
Mheshimiwa alikiri kabisa kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki sijui kauli hii inamaana gani Kama Uhuru wenyewe unatia mashaka! yangu ni hayo ila mamlaka zitoe majibu na zisipotoa basi hakuna uthamani wanauona kwa watu wao!