Uchaguzi 2020 TCRA na Mitandao ya simu mtuombe radhi kwa SMS hii. Mmetoa namba za wananchi kwa wanasiasa? Mmefanya makosa makubwa!

Huu mchezo hawajaanza Leo, Vodacom na Airtel ndo zao. Wamempa access JPM ya database za wateja wao.

Natamani watu waende mahakamani kwa hili ili haya makampuni yalipishwe fidia ya kutosha.
Unataka watu ndo waende wakushtakie? Mtumeni lissu aende kama jambo dogo kama hilo nalo mnashindwa kufungua file, eti nyie ndo mnategemewa kuingia barabarani.
 
Natamani mnaopinga wote muhame nchi muende mkaishi Congo au muende Rwanda mkaishi huko kwa muda fulani.
 
Ukitumiwa utafanya nini!!?
 
Mimi nishawaambia voda na tigo staki sms yoyote ya promotion kutoka kwao, nashukuru walitii mpaka asaiv ni mwaka sijawahi tumiwa sms ya promo kutoka hii mitandao mpaka hizi za Magu sijaona na ndio hata wasijaribu...
 
True
 
Tulizeni munkar, leo mmepokea kutoka CCM ndio mnataka kwenda mahakamani afu wengine wanasema eti kapewa database 😀

acheni utani, hizi meseji za matangazo zipo nyingi sana tu tunatumiwa za makampuni mbalimbali kila uchwao wakitusumbua tu.
 
Mkuu haiko hivyo, taarifa zako zilizoko kampuni za simu ni siri ya wewe na kampuni.Taarifa hizo zikitolewa kwa mtu mwingine bila ridhaa yako ni kosa.Kampuni itatakiwa kutoa taarifa hizo serikali kwa special purpose.kilichofanyika ni makosa.Kitendo cha makampuni ya simu kutoa access ya database za wateja wao kwa wagombea urais au vyama vya siasa ni kosa.Nakuhakikishia kama customers wakalalamika kwa wingi wao na kufungua kesi ni shida
 
Tulizeni munkar, leo mmepokea kutoka CCM ndio mnataka kwenda mahakamani afu wengine wanasema eti kapewa database 😀

acheni utani, hizi meseji za matangazo zipo nyingi sana tu tunatumiwa za makampuni mbalimbali kila uchwao wakitusumbua tu.
Haahaa mkuu hujui.bila database kutolewe hizo SMS zisingeingia kwa wateja kamwe.watalaamu wa it watakubaliana nami
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…