TCRA: Ripoti utapeli kwenye namba 15040

TCRA: Ripoti utapeli kwenye namba 15040

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Mamlaka Ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaomba wanachi kuripoti utapeli wowote unao fanywa kwa njia ya mitandao kwa kutuma aina ya message na namba iliyo tumika kufanya utapeli kwenye namba 15040.

Utapeli huo ni wa Aina yeyote hata ule unao andika "...Ile pesa itume kwenye namba..."

Au utapeli wa Aina yeyote.

MUHIMU! Usibofye linki +unayoishuku iliyotumwa kwa njia ya SMS. Simu yako inaweza kudukuliwa kwa tendo hili. Ripoti utapeli kwa kuituma hiyo SMS kwenye namba 15040.

TCRA
 
Wakati matapeli wanawatumia hata wao TCRA wangekua wapo makini wangewakamata na hizo mambo zisingekuwepo tena...
Haimaanishi kuwa wao hawatumiwi, mbona hata polisi wanaibiwa ila bado wanakamata wahalifu, tena recent kuna traffic police Kenya kaibiwa simu wakati yupo barabarani. Ripoti hizo namba unaweza kuokoa wengi kupigwa
 
Leo nmerpot kenge mmoja ananitumia msg kujifanya Hr wa Tanesco et nataka vijana wawil tu wenye level ya certfcate au dploma nlvyo mwambia we huna ndugu wenye shida ya kaz akaanza matus mfululizo
View attachment 1845280
 
Wana jengo kuuuubwaaa, na landcruiser lenye msufuria mkuuubwaaa juu lakini wanachofurukuta nacho mle ndani hakieleweki
 
TCRA wenyewe ndiyo kikwazo Kwa polisi kitengo Cha Cyber crime kukamata matapeli.

Hawatoi ushirikiano Kwa wakati wanapoombwa taarifa za namba za watuhumiwa wa utapeli.

Wangejikita huko zaidi badala ya huu upotevu wa muda.

Watajaziwa namba za ex wa watu tu.
 
TCRA wenyewe ndiyo kikwazo Kwa polisi kitengo Cha Cyber crime kukamata matapeli.

Hawatoi ushirikiano Kwa wakati wanapoombwa taarifa za namba za watuhumiwa wa utapeli.

Wangejikita huko zaidi badala ya huu upotevu wa muda.

Watajaziwa namba za ex wa watu tu.
Kweli kabisa hapa naona hawajaridhia kabisa kusaidia maana hawana ushirikiano
 
Kumbe yale magari ndo yao
Yalionekana kwenye website yao labda kama wameondoa zile picha maana kipindi cha uchaguzi baadhi ya wadau humuhumu jukwaani walisema yanapikiwa ubwabwa kwa ajili ya wapigakura wa chama dume
 
Back
Top Bottom