TCRA simamieni namba za simu zilizosajiliwa zisipate usajili mpya

Mpalakugenda

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2015
Posts
4,611
Reaction score
5,009
Salam kwenu.

Naona sasa imekuwa kero sana kwa makampuni ya simu kuamua kuzifanyia usajili upya namba simu kwa kigezo hazijatumika kati ya miezi 3 hadi 6.

Leo nimemtafuta mtu kwa namba ta tigo ambayo tulikuwa tukiwasiliana kwa muda mrefu isipokuwa siku za karibuni. Naastaajabu anapokea mtu tofauti.

Kuna siku nimerekebisha simu iliyokufa, niliacha line humo naashangaa haifanyi kazi, naambiwa imepewa usaji kwa mtu mwingine.

Leo pia kuna jamaa analalamika ameenda benk kukopa, anaambiwa namba yake inaonekana alishakopa akatelekeza deni.

Labda TCRA watusadie, ulazima ni upi kuruhusu usajili upya kwa namba ambazo hazitumiki.

Hizi ni identity za watu na ambazo zinaacha alama, tunazungumzua kanzi data binafsi. Sheria yetu inasemaje kuhusu taarifa binafsi.

Fikiria namba yako leo ghafla imetumika na wale jamaa zetu tuma kwenye namba hii.

Soma Pia: TCRA: Utapeli wa "Tuma kwa Namba Hii" umepungua sana nchini

Vodacom Tanzania , Tigo, airtel.

Nadhani mnaweza kufanya kitu, kama namba hazitumiki ni heri mpate consent ya mtu ama mziweke inactive hadi hapo anapoweza kufika katika ofisi zenu na kurudisha tena huduma. Wengine huacha kutumia namba kwa muda kwa sababu tofauti tu.
 
hivi kuna haja ya kutumia namba za tigo au voda kwannn namba ya nida isitumike, nikiishiwa vicha ya voda naweka ya tigo naendelea kupeta
 
Hili jambo kuna haja ya kuzingatiwa sana na hizi mamlaka zilizolala usingizi wa pono,yaani hii nchi kuna watu wanalipwa mishahara lakini hawana tofauti na watu wanaopokea zawadi coz wanachopokea hawakifanyii kazi

Nilisajili line kwa ajili ya Lipa Namba Vodacom imepita mwaka sasa lakini hii line hata leo nimetoka kupigiwa simu na ndugu wa mtumiaji wa mwanzo kila nikijaribu kuwapa sababu za kwanini namba hii ndugu yao alifutiwa usajili hawaelewi.
 
TCRA iboreshe kanuni za usajili wa laini za simu ili kuzuia ukiukwaji wa taarifa binafsi. Kwa mfano, kuweka muda mrefu zaidi kabla ya namba isiyotumika kusajiliwa upya, au kuhitaji uthibitisho zaidi kabla ya kusajili namba upya. Bila hivyo kuna siku mtu atauziwa kesi kwa uzembe wa TCRA
 
Ni usumbufu kweli kweli unaweza fikiria kuitupa line, hivi kama aliyeitumia mara ya kwanza ni jambazi na polisi siku zote wanamtafuta ukiwaambia sio wewe watakubali kweli.
Utapata tabu sana hadi uje uthibitishwe kuwa laini ilipata usajili mwingine.

Kwa mfano mimi nina RB kuna wahuni walinifanyia utapeli namba zao zipo reorted polisi miaka 3 sasa imepita sijaamua kuliamsha tu.

Nawaza siku niamue kupambana na wahalifu wangu tena ambao siwajui majina isipokuwa namba zao tu.
 
Hata Mimi Namba yangu ya Airtel kapewa Mchina.
Hao Airtel nadhani mwezi tu wanaigawa namba. Mie nilishangaa sana line ipo kwenye simu, double line sema yenyewe sikuwa naitumia. Na niliiwekea muda wa maongezi kama buku 5, huwezi amini namba waliigawa. Nawauliza ohh hukuwa unaitumia. Haya rudisheni hela yangu wanambwela tu.
 
Utapata tabu sana hadi uje uthibitishwe kuwa laini ilipata usajili mwingine.

Kwa mfano mimi nina RB kuna wahuni walinifanyia utapeli namba zao zipo reorted polisi miaka 3 sasa imepita sijaamua kuliamsha tu.

Nawaza siku niamue kupambana na wahalifu wangu tena ambao siwajui majina isipokuwa namba zao tu.
Yawezekana kuna gharama kuchonga line mpya ndio maana wanaona ni nafuu kurudia ya zamani.
 
Inathikitisha sana,Kuna dada Whatsap anatumia namba yake ya siku zote Tena kibiashara ila Ukipiga normal call anapokea mtu mwingine.Hata yeye anashangaa ilikuaje namba yake kapewa mtu mwingine kwa muda mfupi wa kutokua hewani.
 
Hili jambo kuna haja ya kuzingatiwa sana na hizi mamlaka zilizolala usingizi wa pono,yaani hii nchi kuna watu wanalipwa mishahara lakini hawana tofauti na watu wanaopokea zawadi coz wanachopokea hawakifanyii kazi

Nilisajili line kwa ajili ya Lipa Namba Vodacom imepita mwaka sasa lakini hii line hata leo nimetoka kupigiwa simu na ndugu wa mtumiaji wa mwanzo kila nikijaribu kuwapa sababu za kwanini namba hii ndugu yao alifutiwa usajili hawaelewi.
Cha ajabu, ikiondolewa kwako hata utake kuirenew utakuta ishauzwa!

Kwa nini namba zinazopokonywa toka kwa wateja ziwe ni tamu sana kugombaniwa kiasi hicho kuliko namba mpya ambazo hazijawahi kuuzwa?

Namba kama namba hazina mwisho, kwa nini wahangaike na namba zilizokwisha kutumika badala ya kuzifuta ama kuzi cease?

Mtoa mada katoa hoja nzuri sana iliyobeba kero kubwa.
 
Yawezekana kuna gharama kuchonga line mpya ndio maana wanaona ni nafuu kurudia ya zamani.
Embu nenda kwa wasajili uone namna line za mitandao ambazo hazijapata wateja zilivyojaa kama takataka.

Cha kushangaza, ukipokonywa leo line yako, kesho ukienda kuifuatilia, unakuta tayari ishauzwa!

Sasa utamu wa kununua namba zilizonyang'anywa toka kwa wateja huwa unatoka wapi?
 
Back
Top Bottom