TCRA toeni adhabu kali kwa baadhi ya redio na TV

Pesanyingi

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2023
Posts
1,157
Reaction score
1,983
Kumekuwa na wimbi kubwa sana la uanzishaji wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini jambo ambalo ni zuri sana.

Ila kutokana na jinsi vyombo hivi vingi vya habari haswa redio na TV zinavyofanya kazi zake nyingi hazina tija katika jamii.

Redio na TV nyingi zimekuwa ni wakala wa kuharibu jamii hasa vijana kupitia vipindi mbalimbali wanavyoandaa.

Redio na TV nyingi wanatangaza sana matangazo ya kubeti(kamari) hii inawaathiri zaidi vijana waache kutafuta maisha kwa njia halali na kuishia kutafuta njia ya mkato kwenye maisha.

Redio na TV nyingi maudhui ya muziki wanaopiga na kuonyesha nyingi hazina maadili zaidi ya ushawishi matendo ya ngono na udhalilishaji wanawake.

Redio na TV nyingi hawana vipindi yenye kuwajenga hasa vijana kuwa timamu kiakili na kuwawezesha kupata mbinu mbali mbali za kupambana kimaisha iwe kiuchumi au kijamii. Zaidi zimejikita kupiga muziki muda wote.
Wito wangu kwaajili ya kulinda vizazi vyetu na Taifa letu baadhi ya vyombo vya habari vifanyiwe kati ya mambo yafuatayo.

1.Vifutwe leseni ya urushaji wa matangazo redio na TV zote zinazo kiuka mila na tamaduni zetu pamoja na wasanii wanao tunga mashahiri yenye kuchochea matendo mabovu kama uvutaji, ngono nk wafungiwe kutokujihusisha na na kazi za sanaa.

2. Vyombo vyote ambayo vimejikita kwenye kutoa burudani tuu peke yake basi kodi zao za uwendeshaji nazo ziwe za juu sana ili visiweze kufikiwa na jamii kwa urahisi zaidi.

3. Redio zote na TV ambazo zitakuwa na maudhui ya kuelimisha jamii, kutunza tamaduni zetu na kutanguliza uzalendo wetu basi kodi yake iwe chini ili wananchi walio wengi waweze kufikiwa.

Tuilinde jamii yetu, vizazi na watoto wetu dhidi ya tamaduni ovu na maudhui hasi kwa faida yao ya baadae.
 
Peleka mawazo ya kijamaa kule
Yaani wasifungiwe wanaotoa vibali vya makampuni ya beti na kuyatoza Kodi
Zije zifungiwe radio wanaotangaza Biashara halali

Hii sio mbinu sahihi ya kudeal na vijana wanaobeting
 
Watangazaji wengi wenyewe wengi mashg mnategemea nn

Ova
 
Back
Top Bottom