TCRA, TRA na Mamlaka zingine za Serikali hazipaswi kulaumiwa

TCRA, TRA na Mamlaka zingine za Serikali hazipaswi kulaumiwa

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Natumaini mko salama.

Leo tena natumia haki yangu ya kikatiba kutoa maoni yangu kuhusu mamlaka za kiserikali hasa zinazolaumiwa zaidi. Kwa muda mrefu Mamlaka hasa TCRA na TRA zimekuwa zikitupiwa lawama wanapofanya kazi zao kwa mujibu wa sheria. Binafsi naona hawastahili kulaumiwa endapo hakuna sheria wanayovunja.

Ikumbukwe sheria hazitungwi na TCRA au TRA bali ni bunge letu. Hivyo sheria mbovu chanzo chake ni bunge. Bunge ndo linastahili lawama. Kwahiyo wananchi tunapoenda kupiga kura tar 28 Oktoba tuhakikishe tunachagua watu wenye angalau elimu kuweza kuelewa miswada inayopelekwa bungeni. Wenye uzalendo pia.

Najua katiba yetu inaruhusu mtu yeyote kugombea ubunge ili mradi ajue kusoma na kuandika lakini wananchi tunaweza kupunguza ukubwa wa tatizo kwa kuwa makini kupiga kura siku itakapofika.
 
Back
Top Bottom