TCRA wakishazima line za simu waje mitaani sasa

TCRA wakishazima line za simu waje mitaani sasa

kagombe

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2015
Posts
3,615
Reaction score
1,805
TCRA wakishazima line za simu waje mitaani sasa kuna kaujanja kanafanywa na hawa vijana wanasajili line mtaani.

Tena ni hatari wanayofanya hawa vijana wasio waaminifu sijui ni tamaa ya pesa au njaa yao.

Hapa tuwe makini tunaokwenda kusajili hapa kuna mchezo wanafanya usipokuwa makini unaweza ukasajilishwa line zaidi ya moja halafu hizo zingine wanabaki nazo wao na kuziuza kwa bei ya juu.

Hii ishu nimeshuhudia mtu anauziwa line kwa bei ya juu na usajili sio wake. Kwa hiyo tuwe makini tuendapo kusajili line zetu ukiona unaambiwa rudia kuweka kidole or hii ile imegoma rudia kuweka kidole utambue unaingia katika kesi.

Ushauri bora twende kwa mawakala wanaofahamika ila sio wapita njia au mtu ana mwamvuli tuwe makini.
 
Hilo suala kiukweli hata Mimi nilibaini kuna mchezo mbaya unafanyika na hawa wasajili line.Ukiona unaambiwa rudia kuweka kidole mara kadhaa ujue unasajilia line watu wengine kupitia kitambulisho chako.Sioni zile za meseji za kitapeli"Tuma kwenye namba hii" zikipotea.
 
Mr. cmp afadhali umesema.
Mimi nikiambiwa niweke kidole mara ya pili nagoma
 
Mimi nilienda ofisi za Airtel nilirudia zaidi ya mara tano. Niwarudie nikawawashie moto?!!
 
Mimi nilienda ofisi za Airtel nilirudia zaidi ya mara tano. Niwarudie nikawawashie moto?!!

Nimenunua line iliyosajiliwa tayari, shida yote ya nini.... asante mkuu huenda ni ya jina lako.
 
Hiyo wazee wa kubet tunasema ni GG Au Both team to score Haijalishi nani kashinda game kati ya walio na namba za NIDA au wasiokua nazo
 
Back
Top Bottom