The Supreme Conqueror
JF-Expert Member
- Feb 13, 2017
- 458
- 1,280
Japo hatua hiyo inaweza kuwa imetokana na sababu nyingine, ukweli kwamba imetokea katika kipindi hiki cha vuguvugu kubwa kuishinikiza serikali iifungie X/Twitter unweza kuyumkinisha kuwa hizi ni dalili za awali za mtandao huo wa kijamii kufungiwa.
Hata hivyo, wakati viongozi mbalimbali wakuu wa kitaifa -Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Spika, kuwataja wachache kati ya wengi -sio tu bado wapo katika mtandao huo wa kijamii bali pia wanaendelea kuutumia, ni uthibitisho kuwa X/Twitter bado ina umuhimu mkubwa kwa Watanzania mbalimbali.
Kichekesho ni kwamba hata “askari wa maadili” walio mstari wa mbele kutaka X/Twitter ifingiwe, wanaendelea kuutumia mtandao huo wa kijamii kufikisha vilio vyao kwa serikali.
Umoja wa Vijana umekuwa mstari wa mbele kuitaka serikali iufungie mtandao huo wa kijamii ikiutuhumu kwamba maudhui yake ni ya ngoni na ushoga na ni kinyume na maadili ya Kitanzania.