TCRA yakaribisha maoni juu ya maboresho ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2018, ili ziwe rafiki

TCRA yakaribisha maoni juu ya maboresho ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2018, ili ziwe rafiki

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewakaribisha Watanzania, kutoa maoni yao juu ya maboresho ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2018, ili ziwe rafiki kwa matumizi.

Wito huo umetolewa leo Jumanne tarehe 11 Mei 2021, Mkoani Morgoro na Mkuu wa Sheria wa TCRA, Dk. Phillip Filikunjombe, katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa mtandaoni, iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).

Dk.Filikunjombe amesema, lengo la mapitio ya kanuni hizo ni kuondoa kanuni ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele na wadau mbalimbali hususan wa habari, kuwa zinakwaza upashanaji habari.

“Watu wa THRDC ni muhimu kuzingatia hili, TCRA imetangaza mapitio ya kanuni. Kulikuwa na nafasi watu watoe maoni kama unaona kuna mahali kanuni iondoshwe na baadhi ziboreshwe, andika maoni kifungu fulani kiondolewe.”

“Sema kifungu fulani kina shida, toa maoni yako, usijiangalie wewe unapotoa maoni, uangalie namna gani kanuni iboreshwe na wafikilie wengine kwa kundi kubwa ili kuona kanuni ziboreshweje. Tunataka kuweka mambo mazuri zaidi,” amesema Dk. Filikunjombe

Akizungumzia mabadiliko hayo, Dk. Filikunjombe amesema, kila nchi duniani, imekuwa ikitumia njia mbalimbali katika kuweka kanuni za matumizi ya maudhui mtandaoni na Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi hizo.

Mwaka 2020, Serikali iliona ije na kanuni za maudhui mtandaoni ikiwemo kuweka utaratibu wa vyombo vya habari mtandaoni, kupata leseni kwanza kabla ya kuanza kutoa huduma au adhabu kwa wakiukaji wa kanuni.

Amesema, lengo la TCRA kuweka kanuni hizo, sio kukandamiza au kubana watumiaji wa mtandaoni, bali lengo la kuratibu matumizi ya mitandao hiyo ili isitumike vibaya katika kukiuka haki za watu.

“Tanzania sio peke yake ina hangaika na uratibu wa ‘social media kwa Tanzania iliona walau tuwe na kanuni na sitaki kusema kama ni nzuri au mbaya lakini walau tuwe na utaratibu.”

“Tulikuwa na maoni kanuni hizi mbaya sana, sheria kandamizi, yawezekana kukawa na matumizi mabaya ya kanuni lakini nia ni njema walau tuwe na taratibu fulani,” amesema Dk. Filikunjombe.

Chanzo: Mwanahalisionline
 
Huku ni kujipendekeza hizi sheria zilipita bungeni na maoni ya watumiaji mtandao yalitolewa sana tu.

#Makamba juniour ndio muasisi wa sheria hizi
 
Huku ni kujipendekeza hizi sheria zilipita bungeni na maoni ya watumiaji mtandao yalitolewa sana tu.
#Makamba juniour ndio muasisi wa sheria hizi
Tulia mzee, tupo awamu ya sita 🤣🤣 ile awamu ndo imeisha hiyo haitakaa irud milele na milele. Sasa mkae kwa kutulia, na tumepiga marufuku kusifu na kuabudu mtu.
 
Safi sana TCRA, hilo ni jambo zuri.

Pendekezo langu.

ONDOENI KANUNI YA KIKUDA ETI WATANZANIA WAKITAKA KUWA NA ACCOUNT YOUTUBE WALIPE SERIKALINI

Hii ni mbaya kwa sababu
1. Serikali hailipi chochote kwa kampuni ya youtube, bali sisi wananchi tunanufaika na elimu, na burudani iliyomo humo. Sasa kwa nini serikali itulimit na sisi kuchangia culture yetu, elimu yetu, ujuzi wetu, burudani zetu kwa ajili ya common good ya familia ya binadamu wote duniani?

2. Kitendo cha kutuwekea ada kuanzisha online channel kule youtube, kunakidhulumu kizazi kijacho kwa sababu kizazi cha sasa kinashindwa kudigitize ujuzi wake, experience yake na kuitunza kwenye server za bure kama hizo za youtube. Kitendo cha kuwa na videos au content nyingi kuhusu maisha yetu ni kwa faida yetu na kizazi kijacho

3. Youtube inaweza kusaidia kuelimisha, kuna vijana wanajua masomo kedekede, hesabu, fizikia, kemia, kompyuta etc, wanvependa kushare ujuzi wao ksma vile wengine duniani wanavyoshare lakini cha ajabu eti serikali inawapiga pini kuwa na channel youtube mpaka Walipe mahela kibao

Binafsi naishukuru TCRA kwa kuwa open minded na kuleta idea hii.

The cyber space must be expanded if we want our nation to keep up a progress pace. Any country that shrinks a cyber space is doomed to be a backwards one. The Chinese government is squeezing the international cyberspace but is smart enough to offer an alternative to its population as far as their local content is concerned, and they are a huge population, so they can mitigate the impact of their authoritarian measure.
 
Hawa wanaregulate YouTube channels za watanzania lakini za nje zinazoonesha mambo ya ajabu ajabu hawana muda Nazi.

Pongezi ziende kwa malaika mtoa roho kwa jinsi alivyoifungua nchi pale Mzena.
 
Sheria kandamizi huwa ni ngumu kuzitekeleza.
 
Hii nchi bwana?

Ina furahisha sana. Yaani waliweka makanuni ya kioumbavu kumfurahisha Jiwe sasa wameona zina wasuta wenyewe.

Njaa mbaya sana. Ni sawa na yule alie kuwa ana tuhadaa uchumi una kuwa kumbe ume poromoka hadi 4%
 
Waondoe leseni za mambo ya maudhui mtandaoni
 
Back
Top Bottom