KERO TCU angalieni upya utaratibu wa vyuo kuwafanyisha wanafunzi mitihani ya online kwa kutumia Moodle

KERO TCU angalieni upya utaratibu wa vyuo kuwafanyisha wanafunzi mitihani ya online kwa kutumia Moodle

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya vyuo kufanyisha wanafunzi mitihani kwa mfumo wa online(Google) na mfumo unakuwa na changamoto nyingi kama vile muda unaowekwa unakiwa hautoshi,unakuta maswali 50 ya kuchagua (mcqs) unapewa dakika 25 yaani ujibu swali moja kwa sekunde 30?

Halafu pia network nyingi nchini sio stable kufanyisha mitihani

Nashauri mamlaka husika zinazosimamia vyuo zifike na kujiridhisha vinginevyo wanafunzi wanateseka sana na Supplimentary zisizo na maana kitu ambacho kinarudisha nyuma morali ya usomaji kwa wanafunzi.
 
Back
Top Bottom