TCU na NACTE ni wepi bora kwa Elimu ya juu Tanzania?

mmaroroi

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2008
Posts
4,635
Reaction score
2,271
TCU na NACTE ni wepi bora kwa Elimu ya juu Tanzania?
 
TCU wanafulia..sijui kwa nini Prof. Nkunya jinsi watu walivyomwamini anatuangusha! Au ameingia uzeeni?? Au siasa?

Nina wasi2 sijui ni Nkunya yule mimi ninayemfahamu na kumheshimu ktk Sayansi Idara ya Chemistry na pia akuwa CACO UDSM!

Kama Nkunya ni member JF basi atupe majibu!
 
Last edited:
Lakini katika selection TCU wako makini kweli kweli.
 
TCU wana mandate gani na NACTE kisheria?

Nacte mbona hawasikiki?
 
Last edited:
TCU wana mandate gani na NACTE kisheria?

Nacte naona ni watu wa hovyo hovyo tu!!
Mzalendo nina doubt kama unafaham unachokisema. TCU wanasimamia vyuo vikuu na NACTE wanasimamia vyuo vya ufundi kama DIT, IFM, CBE na vya binafsi hadi vile vya mafunzo ya kusuka. Kwahiyo ukisema ni watu wa hovyo hovyo, unamaanisha nini?
 
Nacte naijua vizur ila mgeni na tcu. Kiukwel nacte afadhal ya enzi kapuya. Hawana msimamo, elimu imetawaliwa na siasa, utendaji mbovu, mpangilio sio, etc and so on. Take a look masomo kibao alafu kila mwaka module zinabadilika, mfumo alikadharika, mpaka inaboa... Lkn sio kes mana mi mwenyewe ni mwathirika wa nacte.. Kwik.. Kwik.. Natamani kulia. Nadhan wako kifedha zaid. Mtazamo tu jaman..
 
Mzalendo nina doubt kama unafaham unachokisema. TCU wanasimamia vyuo vikuu na NACTE wanasimamia vyuo vya ufundi kama DIT, IFM, CBE na vya binafsi hadi vile vya mafunzo ya kusuka.

Ni kweli wapo tofauti, lakini nimeangalia hii system mpya ya TCU ya udahili nahisi kunaweza kuwa mwingiliano mkubwa tu wa kimajukumu kama hawatakuwa makini.

 
TCU wanasimamia university kama UDSM,SUA,MzUMBE while NACTE wanasimamia Technical College DIT,Mbeya Tech,DMI,NIT
 

becs unasema module unabadilikabadilika zaidi ya kwa Tcu. Nakupa kozi moja ktk udsm nawe unipe mfano wa kubadilika kwa moduli ktk vyuo vya ufundi. Naanza na sheria. Faculty of udsm inaongoza kwa kuwa uncertain in modules,ilianza miaka3,ikaongezewa modules ikapigwa miaka5,ikafa soko wakapunguza mpakamiaka4,wakarudi3, sasa iko 4yrs. Adi watoto wanazeekea digrii ya kwanza, wenzao kama mzumbe wanapeta kiulaini. Juzi kitivo icho icho kimeanzisha B.A in Law enforcement for3yrs,ikiwa na module chache na kwenda field half of 2nd year. Sasa kuanzia next year hii kozi itakuwa miaka4 na kuongezwa modules! Sasa compare uncertainty unayotaka kutoka NACTE,na TCU ktk module za kozi yoyote unayotaka kutueleza!
 

Hapo chacha Nkuu umechema ukweli ntupu bwana wewe. Mie chichemi zaidi hapo. NACTE inamsaidia mtu anayeanza na Certificate kisha akaamua kupandisha madaraja ya elimu hata PhD. Hadi ntu anapata PhD tayari ni nzoefu sana bwana wewe kishule na kiutendaji. Don't you know experience is the best teacher nkuu? Bora NACTE kuliko TCU ambao wanafagilia zaidi freashers from school kupata digirii. Tofauti zao utaziona kazini. Uchimwambie ntu.
 
Nimefuatilia maoni ya wadau,lakini mm
1.ninvyofahamu NACTE wanahusika sana na vyuo visivyokuwa vyuo vikuu (non-universities) na TCU wanahusika na Vyuo vikuu (universities).
2.Kuna tofauti ya kimfumo wa usomaji kati ya nacte na tcu
-nacte wanatumia cbet system (competence based education and training)
-tcu wanatumia kbet system (knowledge based education and training)
3.tcu wanasajili freshers hasa kidato cha sita wakati nacte wanaanzia ngazi ya artisan na
kuendlea.
Nafikiri nitakuwa nimetoa mchango mdogo lakini nafikiri utakuwa umesaidia,
MM NI MHANDISI KUTOKA NACTE!
 
mi nadhan nacte hawako makin maana kuna vyuo vng vya ajab vpo chini yao.....nakumbuka wanafunz wa st.joseph walipeleka barua kutoa taarifa za ubovu wa elimu wanayopewa lakin cha ajab hawajawajbka,,,majengo ya mabat library iko workshop kelele tupu mwaka jana library ilikua haina ceiling board lakin kinapewa dhamana ya kudahili wanafunzi weng kuliko hata DIT walio serious na COET
 
Hizi zote ni mamlaka zenye dhima ya kuinua uelewa kwa vijana wasomi na wanataaluma hapa nchini, TCU=KBET, NACTE =CBET zina jukumu la kumwandaa msomi kuwa na manufaa kwake mwenyewe, taifa na jamii kwa ujumla.
Unapotaka kutambua nani zaidi kati ya hizi taasisi nadhani ungetafuta variable ya mfano ndo ukajanayo hapa.
Kwa mtazamo wangu, TCU wana majukumu yao, kusimamia universities na NACTE kuandaa watendakazi 'mafundi mchundo' bila kujali wanatoka vyuo gani iwe MNMA,DIT, IFM,CBE au hata unavyoviita vya kariakoo,
PASAKA NJEMA
 

Inaonekana huko informed, lakini naomba kutofautiana kidogo na wewe kwenye tofauti uliyoitoa kwenye mfumo wa mitaala ya ufundishaji.
Kwani kwa sasa hivi vyuo vingi especially ndani ya east african countries vinaanza kushift kutoka kwenye kbet system to cbet sytem, so its a matter of time things will be on level ground in terms of curicula systems.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…