TCU na wadau wengine wa elimu( masters and PhD za SUA zinatesa wasomaji)

yaasary

Senior Member
Joined
Mar 26, 2011
Posts
110
Reaction score
59
Ndugu zanguni, hizi masters na PhD za SUA kwa kweli inakuwa ni mateso kwa wasomaji yaan course duration mfano kwa masters degree ni miaka miwili lakin imekuwa ni suala la kawaida kwa mtu kutumia up to 4 and 5 years, na kwa PhD hadi miaka 7,8, 9, mfano kwa mahafali ya 29 ya mwaka huu Msc of crop science wamemaliza watu 34 lakin ni mtu mmoja tu ambaye amesoma kwa mda muafaka ( kwa miaka miwili), jamani hivi hili swala ni la kawaida na kwa vyuo vingine vinavyotoa masters za natural science mfano UDSM, niliongea na mwanafunzi mmoja wa masters ambaye naye ameshindwa kumaliza mwaka huu na hivyo anaelekea mwaka wa tatu sasa akisoma masters, anasema tatizo ni kuwa wakufunzi hawapitii research za wanafunzi kwa mda unaotakiwa yaani wanatumia mda mrefu sana kukaa na kazi hivyo kusababisha ucheleweshaji wa kufanya marekebisho, Jamani hivi tume ya vyuo vikuu (TCU) haina mamlaka ya kuangalia hili swala
 
majanga! sio kwamba wanafunzi ndio vilaza kwa kushindwa kufanya utafiti au kuandika theses kwa ufasaha unaotakiwa? nadhani na ukilaza wa wanafunz unachangia--iweje wengine wahitimu kwa wakati na wengine wachelewe? kuna jamaa zangu wawili wanachukua masters SUA huu mwaka wa 3 hawajahitimu lakini ni kwa 7bu ya uzembe wao wala sio kosa la wahadhiri--ni UZEMBE wao tu!
 

ndugu yangu wacha kabisa SUA anakufa daktari anapona mgonjwa, mimi hapa sineni neno karibu idara ninayosoma, sijawahi kwenda likizo wala wikiendi kila siku kiguu na njia librari lakini naogopa hata kusema nipo mwaka wa pili, maana historia idarani kwetu hapa inaonyesha ukihitimu ndani ya miaka mitatu ni mojawapo ya bahati kubwa kwako, wengi wanaenda mpaka miaka mitatu, minne na mitano, inaumiza kweli hasa ukichukulia wafadhili wetu wanajua shule ni ya miaka miwili tu! watu wanahitimu masters kwa miaka mitano wanafikiri ni PhD kumbe bado ni uzamili tu!
 

Uko sahihi chief nilisoma masters hapo kwa miaka 3 kwa upuuzi wa supervisor japo nimerudi pia kwa PhD ni kwa matakwa ya mfadhili tu but kuna walio wazuri mfano Prof Mvena jamaa yangu alibahatika kumaliza kwa wakati
 

hapana mkuu, ukichukulia mfano wa faculty of agriculture watu wengi wanaochukua degree ya pili pale SUA huwa wamechukuwa degree ya kwanza palepale na kwa jinsi ninavokijua kile chuo kwa upande wa utafit wako makini sana yaani mtu akimaliza first degree pale anakuwa ameiva kwelikweli kwa kufanya utafiti na kwa kawaida kama mtu anajijua yeye ni mzembe huwa harudi for masters pale bali anaenda chuo kingine, hao jamaa zako labda first degree hawakuchukulia SUA, tatizo la pale ni ukiritimba wa wakufunzi, halafu jamaa wako busy sana na kufanya research zao sa mi najiuliza kwa nini mtu asiende tu kwenye agricultural research institute akafanye utafiti huko mwaka mzima kuliko kuzingua wanafunzi chuoni
 
Kutokumaliza MSc au PhD huko SUA na vyuo vingine vingi vya mchepuo wa sayansi kunasababishwa na sababu nyingi na sio kuangusha lawama zote kwa masupervisors.

Kwanza inawezekana mwanafunzi ni mzembe, au sio mzembe ila ana mambo mengi, mara nyingi wanafunzi wa huku juu wanakuwa na majukumu mengi maana ni watu wazima kwa hiyo unakuta hawatengi muda wa kutulia kufanya tafiti na kuandika tafiti nzuri. Hii inapelekea wanafunzi wengi kutengeneza data zinawapa wakati mgumu kuzianalyze na kuandika majibu vizuri. Kupitia huko husababishia hata supervisor nae kupata tabu sana kusoma na kuelewa kazi ya mwanafunzi, unakuta supervisor anachukua muda mrefu sana kuinyoosha kazi ya mwanafunzi kazi ambayo kiukweli alitakiwa kuifanya mwenyewe akiwa ametulia. Pia wanafunzi wajue kusoma kazi ya mtu inategemea pia na hamasa yaani namaanisha uandikaji wa mwanafunzi, ni kama vile unavyosoma hadithi kama mwandikaji anamtiririko vizuri,msomaji unapata hamasa zaidi.


Pia kuna tatizo la walimu ambalo wengi mmegusia, hakika ni kweli kuna aina ya walimu hawatumii muda wao kumsaidia mwanafunzi kuanzia mwanzo wa kufanya tafiti na hii inapelekea kugundua mwanafunzi amefanya tafiti wakati muda umeshapita na inakuwa ngumu kurekebisha. Pia hata akipelekewa kazi asome basi itamchukua muda mrefu kuisoma kwa sababu ya kuwa na mambo mengi nje ya tafiti, walimu siku hizi wamekuwa busy kufanya kazi za part time vyuo vingine, unakuta mwalimu anafundisha zaidi ya vyuo 5.

Mbali na sababu ya wanafunzi na walimu wao, sababu nyingine ni aina ya tafiti yenyewe, kiukweli kuna tafiti zinahitaji muda mrefu na zinachamoto nyingi ambazo mtafiti anakutana nazo, mfano kwa wale wa kilimo unakuta magonjwa unaharibu na kuchelewesha umalizaji na upataji wa majibu katika muda muafaka

Sababu nyingine ni upatianaji wa vifaa ambavyo wanafunzi wanahitaji kwenye tafiti, vingi na vya kuagiza nje ya nchi. Wakati mwingine mwanafunzi hawezi kuendelea na tafiti akingojea kifaaa au chemical kwa zaaidi ya mienzi sita.

Kwa Sababu hizo ni ngumu kwa wanafunzi kumaliza kwa muda wa miaka miwili, na hii sio SUA bali ni vyuo vingi vya sayansi, Tanzania na Afrika kiujumla
 

Yap mkuu nimekusoma sababu ulizozitaja naona zina mashiko, ila inauma sana pindi inapokuwa mwanafunzi anajuhudi but mkufunzi ni mzembe
 
Inaonekana hapo SUA elimu ni ngumu na pia urasimu wa wahadhiri..
 

Ulitumwa Uende Hapo? Shift to Other Varsities Please!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…