TCU rekebisheni hii kasoro

TCU rekebisheni hii kasoro

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Tunashukuru TCU hatimaye wametoa majina ya waombaji waliochaguliwa kwenye chuo zaidi ya kimoja na wahusika wanatakiwa wa-confirm chuo wanachokitaka. Tatizo ni kuwa hawajaainisha kozi alizochaguliwa kwenye kila chuo maana mwombaji alikuwa anaomba zaidi ya kozi moja kwenye kila chuo. Kwa taarifa ya TCU waombaji bado hawajajua wamechaguliwa kozi zipi. Cha maana zaidi ni aina ya kozi wala siyo chuo maana chuo utakiacha lakini kozi ndiyo itakayohusika na maisha yako. Haiwezekani mtu aka-confirm chuo wakati hajui ni kozi ipi amechaguliwa huko kati ya zote alizozichagua. TCU fanyieni update taarifa yenu ili iainishe kozi pia aliyopata kwenye kila chuo alichochaguliwa.
 
BonGo nyoso kitambo sana, tunakurupuka tu
 
Chuo husika ukiingia kweny account yko wanakwambia kozi uliyochaguliwa
Screenshot_20180902-014433.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kiukweli huo ndo ukweli. vyuo pia vingetoa majina kama mwaka jana. suala la kuangalia kwenye akaunti lina utata. kwa mfano ardhi university hadi sasa akaunti zao hazifunguki zinaandika aplication still in progress. suala la kozi ni muhimu kuainisha
 
alieconfirm saut anichek nimwelekeze kila asichokijua na maisha mazima pandeza mwanza
 
Vyuo vingine viige mfano wa udom. watoe orodha ya wanafunzi wao...
 
Me nldhani MTU anapo select chuo ana select na course sasa iweje usijue course ya chuo ambacho umedelect we mwenyewe wadau au me ndo sielewi.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TCU ingilieni kati vyuo vyote viweke list wazi ya wote waliochafuliwa huko na kozi zake. tarehe 5 sio mbali...
 
Back
Top Bottom