TCU shughulikieni tatizo CAS.

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kwa waliojaribu kuitumia CAS wanaelewa kero mbali mbali za hii sytem.Kwa mfano kwenye profile yako baadhi ya taarifa hazionekani licha ya kuwa umeiziingiza kwa usahii kabisa,au unaweza kuclik selected program kwa lengo la kubadilisha kozi badala yake system inakurudisha nyuma kwenye page ya home/registration wakati ulishakamilisha hatua hiyo.Tatizo lingine kwa mfano leo asubuhi ukiingia kwenye website inafunguka vizuri ila ukija click kwenye option ya click to apply yanatokea maneno this site is hacked.

Swali hapa hawa maofisa wa TCU wanafanya nini kuondoa tatizo hili?Mbona matatizo haya ni ya muda sasa na wako kimya tu?Wanataka muda uishe alafu watu wapate hasara?

Jamani hembu wajibikeni hata kwa kutoa ufafanuzi kuliko kukaa kimya wakati tunapata shida hii.
 
C I T bongo hamna kitu. Wataalam serikalini wako busy na kucheza karata badala ya kuboresha mtandao wao
 
System iko poa check computer yako mkuu me nme tumia mbona iko mwake
 
Salary slip,kama unafanya applcation kwenye simu usishangae. Mimi mwenyewe nilikuwa nikifanya kwenye simu ikawa inaniletea matatizo kama hayo(nilipokuwa najaza program codes),nikaenda cafe(kwenye Computer) ndo ikakubali.
HESLB nao vivyo hivyo,niliingia internet cafe moja(wana desktop comp.old modern). Katika kujaza 'birth date',nikakuta miaka kuanzia 1940 hadi 1987 tu! Nilipoenda kwenye cafe nyingine(town) nikafanikiwa bila matatizo.
Hadi sasa nashindwa kutazama "Selected programs" kwa kutumia simu yangu.Baada ya kulogin,nikiclick "Selected Programs" inalogout yenyewe.
NENDA CAFE TOFAUTI NA JARIBU,AU TUMIA COMPUTER NYINGINE UTAFANIKIWA.
 
Last edited by a moderator:
HESLB ndo tabu tupu - kila ukijaza Transaction ID unaambiwa Transaction does not exist - hii ni tokea jana: OLAS :M-PESA Transaction - M-PESA Transaction ID does not Exist
 
Hah! Nimeona tena utakuja ameuliza swali kama hilo hilo! Mimi nilijaza pia tangu tarehe 16 april,na haikuwa na shida yeyote. Labda basi kwa sasa ndo inazingua.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…