TCU wasaidieni wanataaluma wa SUZA

TCU wasaidieni wanataaluma wa SUZA

Mutakkalim

New Member
Joined
Nov 2, 2022
Posts
2
Reaction score
0
Ni kuhusu kadhia ya kutokupandihswa madaraja kwa wanataaluma. Suala la academic promotions kwa chuo kikuu cha taifa cha Zanzibar (SUZA) ni la kusikitisha na kufedhehesha.

Mchakato unachukua muda sana kiasi ambacho mwanataaluma anaweza kuomba promotion ikachukua mwaka na zaidi bila ya kujuulishwa tatizo ni nini, jambo ambalo linaenda kinyume na academic promotion guidelines.

Mfano mzuri ni mwaka uliopita wa masomo, wanataaluma walituma maombi yao mnao April wa mwaka huu, lakini hadi sasa hakuna taarifa yoyote kuhusu promotions.

Inakuaje vyuo vyengine vyote TZ vinatoa pdf kuwatangaza wale waliokidhi promotions lakini hilo halifanyiki kwa SUZA.

TCU tunaomba mufatilie hii issue wanataaluma wapate haki yao stahiki.
 
Back
Top Bottom