TCU yaongeza muda wa Udahili wa Shahada ya Kwanza katika Programu zenye nafasi 2024/2025

TCU yaongeza muda wa Udahili wa Shahada ya Kwanza katika Programu zenye nafasi 2024/2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
1.0 UTANGULIZI Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inaufahamisha umma, Taasisi za Elimu ya Juu na wadau wa Elimu ya Juu ndani na nje ya nchi kuwa udahili katika awamu zote mbili kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2024/2025 umekamilika. Majina ya waliodahiliwa katika Awamu ya Pili yatatangazwa na vyuo husika tarehe 05 Oktoba, 2024.

2.0 WAOMBAJI WALIODAHILIWA KATIKA CHUO ZAIDI YA KIMOJA
Waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Pili na wale ambao hawakuweza kuthibitisha udahili katika Awamu ya Kwanza, wanapaswa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia tarehe 05 hadi 21 Oktoba, 2024.

Uthibitisho huo unafanyika kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili. Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika.

Aidha, uthibitisho wa udahili ufanyike kupitia akaunti ambayo muombaji alitumia wakati wa kuomba udahili. Kwa urahisi wa rejea, orodha ya majina ya waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja itapatikana kwenye tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz) tarehe 05 Oktoba, 2024.

3.0 KUFUNGULIWA KWA AWAMU YA TATU YA UDAHILI 2024/2025
Baada ya kukamilika kwa awamu zote mbili za udahili, Tume imepokea maombi ya kuongeza muda wa kutuma maombi ya udahili kutoka kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), baadhi ya waombaji ambao hawakufanikiwa kupata udahili katika awamu zilizopita na pia vyuo ambavyo bado vina nafasi vimeomba vipewe muda kuendelea kudahili.

Hivyo, Tume imeongeza muda wa udahili kwa kufungua Awamu ya Tatu na ya mwisho ya udahili itakayoanza tarehe 05 hadi 09 Oktoba, 2024. Tume inawaasa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakuweza kupata nafasi ya kudahiliwa katika Awamu ya Pili kutokana na sababu mbalimbali, watumie fursa hii vizuri kwa kutuma maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda.

Aidha, Tume inaelekeza Vyuo vya Elimu ya Juu nchini kuendelea kutangaza programu ambazo bado zina nafasi. Waombaji udahili na vyuo wanapaswa kuzingatia utaratibu wa udahili wa Awamu ya Tatu kama ilivyoainishwa katika Jedwali.

Jedwali: Utaratibu wa udahili katika Awamu ya Tatu kwa mwaka wa masomo 2024/2025

4.0 WITO KWA WAOMBAJI UDAHILI
Waombaji udahili wa Shahada ya Kwanza wanakumbushwa kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo kimoja yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika. Kwa wale ambao watapata changamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa.

Imetolewa na:
Prof. Charles D. Kihampa
KATIBU MTENDAJI
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA


WhatsApp Image 2024-10-04 at 12.02.16_e5b2d850.jpg

WhatsApp Image 2024-10-04 at 12.02.16_aa8259cd.jpg
Soma:
~
TCU yafungua dirisha la udahili kwa waombaji wa vyuo vikuu kwa Mwaka 2024/25
~ Matokeo Kidato cha Sita 2024 yatoka. Ufaulu wapanda kwa asilimia 0.26
~ Matokeo Kidato cha Sita 2024
 
Dah watu wanasoma ila huku mtaani ni kugumu jmn nataman serikali iwekeze nguvu kwenye ufundi kuliko huku kwenye vyuo vikuu utakuta mtu anaenda kusoma kozi haielewek tena miaka mitatu dah very sad
 
Back
Top Bottom