Teak Wood Tree - Loan

Teak Wood Tree - Loan

Kilimo Kwanza

Member
Joined
Jul 20, 2010
Posts
49
Reaction score
20
Habari wajameni.
Nasikia wakulima wa miti ya mitiki(Teak) huko moro wanaongelea CRDB bank wanatoa mikopo kwa dhamana ya hiyo miti, wanasema miti yenye umri wa kuanzia miaka 3 na kuanzia hekari 1 wanakupa mkopo.
Je Kuna yo yote anayefaham km hili jambo ni kweli?
 
Mkuu hii kitu inawezekana kama utakuwa na tittle deed ya shamba lako plus an operating business.
Pia kama shamba lako ni large scale basi nenda pale sua kuna mhadhiri anaconnection na shirika flani marafiki wa mazingira kutoka canada wanatoa mkopo mrefu na mnono kwelikweli kiasi kwamba utamu wa kupanda miti utaufaidi mpaka siku ya mavuno ya mitiki hakika utakuwa umekinai.
Kesho ntajongea CRDB nikajihakikishie mwenyewe then nilete mrejesho kamili hapa jukwaani.
 
Poa poa, nashukuru kwa taarifa hizi mkuu.
Nasubiri hizo taarifa za CRBD hiyo kesho.
Mi naishi Dsm, we unaishi Moro?
 
Mkuu hii kitu inawezekana kama utakuwa na tittle deed ya shamba lako plus an operating business.
Pia kama shamba lako ni large scale basi nenda pale sua kuna mhadhiri anaconnection na shirika flani marafiki wa mazingira kutoka canada wanatoa mkopo mrefu na mnono kwelikweli kiasi kwamba utamu wa kupanda miti utaufaidi mpaka siku ya mavuno ya mitiki hakika utakuwa umekinai.
Kesho ntajongea CRDB nikajihakikishie mwenyewe then nilete mrejesho kamili hapa jukwaani.

mkuu maelezo yako mazuri ila huko kwenye kimombo kote sijaelewa kwa kweli.
nitarudi kama utarekebisha
 
mkuu maelezo yako mazuri ila huko kwenye kimombo kote sijaelewa kwa kweli.
nitarudi kama utarekebisha

Namaanisha kuwa kama utahitaji mkopo kwenye benki kupitia shamba la mitiki kama dhamana, ni lazima shamba lako liwe na hati miriki. Pia lazima uwe na mradi wa biashara inayojiendesha na kutamburika kihalali; Yaani uwe na TIN # na leseni ya biashara ili wajue namna utakavyokuwa unarejesha huo mkopo na riba yao. Umeelewa mkuu SuperH?
 
Last edited by a moderator:
Mrejesho CRDB.
Wakuu jana nilienda bank kuulizia mkopo kwa collateral ya shamba la mitiki;
Ni kweli kuwa wanatoa mkopo kuanzia shamba la ekari moja, miti iwe atleast miaka mitatu na iwe na hata angalau hati ya kimila.
Kikubwa zaidi ni kwamba unatakiwa uwe na biashara ambayo itamudu kurejesha mkopo na uzuri zaidi ni kwamba wanatoa mkopo mkubwa kulingana na ukubwa wa shamba lako, umri wa miti na uhitaji wako wa mkopo.
Nihayo tu waungwana HIMA SASA NA TUPANDE MITI kwa maendeleo yetu na kujenga mazingira rafiki na hali ya hewa ya uso wa Dunia.

CC; Kilimo kwanza Super H Marire Gloryvanessa forum na wapendwa wote ndani ya jukwaa letu.
Samahani sana kwa kuchelewesha mrejesho.
 
Last edited by a moderator:
nimeelewa mkuu. Kisima

Haina shaka mkuu sana Marire, twende sasa tukapande miti ndugu zangu tusiiachie fursa hii adhimu kabisa kwa mstakabari wa maendeleo yetu maana wazee wetu na hata baadhi ya vijana wenzetu wamekuwa waoga kujikita kuwekeza kwenye upandaji miti kwa kuhofia return on investiment.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu.. Kisima, asante sana!
Hii ndio niliyokuwa naitaka.
Sasa kazi kwetu wajasiri amali.
 
Mkuu.. Kisima, asante sana!
Hii ndio niliyokuwa naitaka.
Sasa kazi kwetu wajasiri amali.

Hili ni suruhisho tosha kwa wajasiriamali tusio na mitaji na tuna aim higher! Kumbe ni rahisi sana kukuza mtaji kwa kupanda mitiki ekari tatu after three yrs unajongea CRDB kuapply loan zaidi ya milioni 50!
Tushindwe nini sasa jamani Bongo tambarare sana nikujipanga tuuu!!!
 
Kwa hiyo ukishindwa kufanya marejesho wanakamata shamba au niaje
 
Kwa hiyo ukishindwa kufanya marejesho wanakamata shamba au niaje

Mkuu Mzururaji ndiyo maana unashauriwa ujiridhishe kwanza na project au biashara unayoenda kufanya kama itahimili marejesho. Hata hivyo naamini kuna namna negotiation inafanyika kabla hujapewa mkopo na inategemea na kiasi cha pesa ulichochukua.
Haiingii akilini umekua granted loan ya milioni 5 kwa hekari 30 za mitiki then ukashindwa kurudisha mkopo wakataifisha shamba.
Mhimu ni kuondoa woga ukishajikita kwenye ujasiriamali pambana!!
 
Last edited by a moderator:
Hii ni fursa nzuri sana,ila ni kuomba Mungu wasije wakabadilikia njiani,maana kupanda mitiki kwa mwaka 2014 maana yake mkopo ni 2017 kitu ambacho si kibaya na wala si muda mwingi iwapo hawatabadili masharti yao!je wadau mnaweza kunipa mwanga miteak inastawi zaidi katika maneo au hali ya hewa ya namna gani?na kwa Morogoro ni ukanda upi inaweza kustawi zaidi?
 
mkuu. 1800 unaweza kusachi hapo juu kuhusu mitiki kuna nyuzi kibao huko jf zimechambua hiyo miti hadi utapenda!
 
Last edited by a moderator:
Hii miti nilianza kuifaham pale ofc za mbegu moro. Dada mmoja wakati naongea naye aliniambia, "mimi nina hekari 4 za miti yenye umri wa miaka 2 tu, juzi kuna mfanyabiashara alinifwata akitaka anipatie milioni 80 lkn nilikata"... Daahh, kuanzia pale akili ikaanza kunienda resi kuhusu hichi kilimo.
 
Mkuu, fanya unitumie contact za huyo dada na jamaa yake aliyetaka kununua hiyo mitiki. Huku niliko kuna mashamba mawili ya mitiki yapo sokoni tena kwa bei nzuri ajabu!
Lipo shamba la ekari 4 na ekari 6 na miti yake ina zaidi ya miaka mitano. Nakuomba ufanye hivyo mkuu make ni muda sasa hawa watu wanahaha niwataftie wateja!
 
Hii ni fursa nzuri sana,ila ni kuomba Mungu wasije wakabadilikia njiani,maana kupanda mitiki kwa mwaka 2014 maana yake mkopo ni 2017 kitu ambacho si kibaya na wala si muda mwingi iwapo hawatabadili masharti yao!je wadau mnaweza kunipa mwanga miteak inastawi zaidi katika maneo au hali ya hewa ya namna gani?na kwa Morogoro ni ukanda upi inaweza kustawi zaidi?

Kwa morogoro ni ukanda wa Kilombero na Ulanga, kwa kilombero ni hasa maeneo ya Ifakara.
[h=3]Kilombero Valley Teak Company Limited | Global ...[/h]
 
Back
Top Bottom