Kilimo Kwanza
Member
- Jul 20, 2010
- 49
- 20
Tunakusubiri mkuu maana naona siku imeshaanza @je bado uko crdb....
Mkuu hii kitu inawezekana kama utakuwa na tittle deed ya shamba lako plus an operating business.
Pia kama shamba lako ni large scale basi nenda pale sua kuna mhadhiri anaconnection na shirika flani marafiki wa mazingira kutoka canada wanatoa mkopo mrefu na mnono kwelikweli kiasi kwamba utamu wa kupanda miti utaufaidi mpaka siku ya mavuno ya mitiki hakika utakuwa umekinai.
Kesho ntajongea CRDB nikajihakikishie mwenyewe then nilete mrejesho kamili hapa jukwaani.
mkuu maelezo yako mazuri ila huko kwenye kimombo kote sijaelewa kwa kweli.
nitarudi kama utarekebisha
Mkuu.. Kisima, asante sana!
Hii ndio niliyokuwa naitaka.
Sasa kazi kwetu wajasiri amali.
Kwa hiyo ukishindwa kufanya marejesho wanakamata shamba au niaje
Hii miti nilianza kuifaham pale ofc za mbegu moro. Dada mmoja wakati naongea naye aliniambia, "mimi nina hekari 4 za miti yenye umri wa miaka 2 tu, juzi kuna mfanyabiashara alinifwata akitaka anipatie milioni 80 lkn nilikata"... Daahh, kuanzia pale akili ikaanza kunienda resi kuhusu hichi kilimo.
Hii ni fursa nzuri sana,ila ni kuomba Mungu wasije wakabadilikia njiani,maana kupanda mitiki kwa mwaka 2014 maana yake mkopo ni 2017 kitu ambacho si kibaya na wala si muda mwingi iwapo hawatabadili masharti yao!je wadau mnaweza kunipa mwanga miteak inastawi zaidi katika maneo au hali ya hewa ya namna gani?na kwa Morogoro ni ukanda upi inaweza kustawi zaidi?