TEC yatahadharisha matumizi ya Akili Mnemba (AI ) dira 2050

TEC yatahadharisha matumizi ya Akili Mnemba (AI ) dira 2050

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Kueleka mwaka 2050 serikali ya Tanzania imehimizwa kuweka lengo la kuhakikisha kuwa kunakuwa na muongozo sahihi wa matumizi na ulinzi ya akili mnemba (Artificial Inteligence) ili kuhakikisha kuwa kama taifa linajilinda dhidi ya hatari mbalimbali zinazoweza kuibuka kwenye matumizi makubwa ya kiteknolojia kwa miaka 25 ijayo.

Bi Mariana Balampama, Mjumbe mshauri wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) amezitaja hatari za Akili Mnemba kuwa ni pamoja na wingi wa taarifa potofu, kuvuja kwa taarifa binafsi pamoja na masuala ya ulinzi na usalama wa nchi.

Ametoa kauli hiyo Jumatatu, Januari 13, 2025, katika Mkutano wa Kamati ya Dini Mbalimbali Kuhakiki Rasimu ya Dira hiyo, uliofanyika Ukumbi wa TEC, Kurasini, Dar es Salaam, ikiwa ni Kundi la Mwisho kufikiwa na Tume ya Mipango kwaajili ya Mapitio ya rasimu hiyo.

 
Back
Top Bottom