Tech & media convergency (TMC) yashirikiana na Ubalozi wa Marekani dar, katika kutekeleza mradi wa kuimarisha ushirikiano katika ajenda ya kidijitali

Tech & media convergency (TMC) yashirikiana na Ubalozi wa Marekani dar, katika kutekeleza mradi wa kuimarisha ushirikiano katika ajenda ya kidijitali

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Dar es Salaam, 16 Januari, 2025 - Tech & Media Convergency (TMC) Inapenda kuwatangazia ushirikiano wake na Idara ya Serikali ya Marekani (Ubalozi wa Marekani, Dar es Salaam) katika kuzindua Mradi wa kimapinduzi ya Tanzania Digital Collaboration."

Programu hii ya kibunifu unalenga kuimarisha utawala wa kidemokrasia wa kidijital, kukuza uelewa wa vyombo vya habari, kuboresha usalama wa mtandaoni, na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau mbalimball, wakiwemo viongozi wa sekta ya teknolojia, watunga sera, wataalam wa vyuo vikuu, na mashirika ya kiraia kote Tanzania.

Ushirikiano huu unaimarisha dhamira ya TMC katika mpango mkakati wake wa miaka mitano (2024-2026) na kuimarisha ajenda ya Utawala wa Mtandao nchini Tanzania. Mpango huu unalenga kukuza ushiriki wa raia katika teknolojia, kushughulikia changamoto za usalama wa mtandao na ulinzi wa data binafsi, kupunguza vitisho vya kidijitali kwa miundombinu muhimu, kushughulikia uadilifu wa taarifa, na kutetea mfumo wa utawala wa kidita jumuishi na wa usawa
Mambo Muhimu ya Mradi Huu
Mradi huu utahusisha mikoa 8 nchini Tanzania, na unatarajiwa kuwafaidisha moja kwa moja zaidi ya watu 2,000 na kwa njia isiyo ya moja kwa moja zaidi ya watu 5,000.

Vipengele vikuu vya mpango huu ni
• Utetezi wa Sera na Ushirikiano wa Wadau ili kuleta mabadiliko makubwa katika utawala wa kidijitali
• Kukuza ukuaji wa Kiuchumi kupitia programu za kubadilishana maarifa, ushirikiano wa kimataifa, na utaalam wa Marekani
• Kuimarisha Mashirika ya Kiraia kuongoza juhudi za Utawala wa Mtandao na Ushirikiano wa kidijital
• Ushirikiano na Uwezeshaji wa Jamii na Wadau wa kimkakati kupitia mafunzo, warsha, na programu za kujenga uwezo.
.
• Utafiti Kuhusu Utawala wa Mtandao na Haki za kidijitali kusaidia utungaji wa sera unaotegemea ushahidi.
Kwa kutumia majukwaa ya kidijitali, Mradi huu utashughulikia changamoto kama taanfa za upotoshaji, ukosefu wa ujuzi wa kidijitali, na udhaifu wa usalama wa mtandao, hivyo kuiweka Tanzania katika nafasi ya kuwa kinara wa sera za teknolojia bunifu na jumuishi
Kwa Nini hivi sasa?

Licha ya maendeleo ya kidijitali nchini Tanzania, bado kuna mapengo makubwa katika kushirikisha maoni ya umma na mashirika ya kiraia katika usimamizi wa TEHAMA. Ukosefu wa mfumo wa ushirikiano jumuishi ambao unahusisha viongozi wa sekta ya teknolojia, watunga sera, vyombo vya habari, wataalamu wa vyuo vikuu, na mashirika ya kiraia-umeathiri uwezo wa taifa kukabiliana na changamoto kama usalama wa mtandao, utawala wa kidemokrasia wa mtandao, ulinzi wa data binafsi, na upatikanaji wa rasilimali za kidijitali kwa usawa Mpango wa Tanzania Digital Collaboration" unalenga kuziba mapengo haya kwa kukuza ushirikiano, kuongeza uelewa wa umma, kuimarisha uadilifu wa taarifa, na kuwawezesha mashirika ya kiraia kushiriki kikamilifu katika kuunda mustakabali wa kidijitali wa Tanzania
Kuhusu Tech & Media Convergency (TMC)
TMC ni mtetezi mkuu wa Utawala wa Mtandao na mabadiliko ya kiteknolojia nchini Tanzania.

Ilianzishwa mwaka 2021, dhamira ya TMC n kuendeleza jamii inayotegemea maarifa kupitia mikakati ya TEHAMA, Utawala Bora wa Mtandao, na uvumbuzi wa kidijitali. Shirika hil limekuwa likifanya kazi mara kwa mara kuimarisha ushiriki wa raia, usalama wa mtandao, na sera za kidijitali jumuishi
TMC ni mwanachama wa mitandao ya kimataifa, kiwa ni pamoja na
⚫ITU's Partner 2Connect Digital Coalition

• National Democratic Institute's Global Info/tegrity Network
• UN Women ESARO's Regional Civil Society Advisory Group
• East Africa Internet Governance Forum (EAIGF) and Africa Internet Governance Forum (AFIGF)
• Internet Governance Tanzania Working Group (IGTWG)
Kuhusu Mradi wa Ushirikiano wa Kidijitali Tanzania (Tanzania Digital Collaboration)

Balozi ya Marekani jijini Dar es Salaam, kwa kushirikiana na Idara ya Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ilbuni programu hii kupitia mchakato wa ushindani ulio lengo la kuhamasisha Uchumi wa Kidijital wa Tanzania na kuchochema mageuzi ya kina ya kidijitali nchini. Programu imeundwa ili kuchagiza na kukuza Uchumi wa Kidijitali na kuwekeza Jitihada za kushirikiana na Asasi za Kirala, Wadau husika kwa kubadilishana maarifa, ushirikiano wa kimataifa, na utaalamu wa Wataalam kutoka Marekani.

Programu hii inalenga kuwawezesha wabunifu wa Tanzania, watunga sera, asasi za kiraia, na vyombo vya habari kuhimiza maendeleo ya miundombinu ya kidijitali inayochochea maendeleo endelevu ya kiuchumi huku ikilinda haki na uhuru wa mtu binafsi, Inasisitiza uundaji wa mazingira na mifumo ya kidijitali inayoshirikiana, inayoweza kutegemewa, na iliyo salama huku ikilinda jamii, na kuhakikisha uwepo wa uadilifu wa taanfa na habari na kuimarisha utawala wa TEHAMA
Matarajio ya Baadae
Mradi wa Tanzania Digital Collaboration" unalenga kufafanua upya mazingira ya kidijitali ya Tanzania, ukitoa mfano wa utawala wa kidemokrasia na jumuishi katika enzi ya kidijital.

Kwa kuzingatia ushirikiano, uvumbuzi, na uwezeshaj, TMC inakaribisha washirika na wadau kuungana katika kujenga mfumo thabiti na wa usawa wa kidijital kwa wote.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana nasi
E info@mediaconvergency.co.tz.www.tmc.co.tz
IMG-20250116-WA0197.jpg
 
Back
Top Bottom