Technology: Maana ya cryptocurrency, metaverse na nft

Technology: Maana ya cryptocurrency, metaverse na nft

UBILUKO

Member
Joined
Sep 30, 2018
Posts
94
Reaction score
192
Watu wengi nimekuwa nikisoma thread zao humu kuhusiana na cryptocurrency, METAVERSE na NFT

Nimegundua vitu vifuatavyo

1. Watu wengi wamepitia changamoto nyingi sana katika utafutaji wao hasa online Hustler kiasi kwamba wameibiwa pesa zao na Kisha kupoteza matumaini Tena za vitu vyovyote vinavyohusu kuingiza kipato kwa njia za mitandao wakiamini ni scarm(utapeli)

2.watu wengi wanashida ya lugha

Yaani vitu vingi vinavyohusu utengenezaji wa pesa mtandaoni au vya kiteknolojia maelezo/mafunzo yake hupatikana kwa lugha ya kiingereza kitu ambacho kinachangia mtu kutofanya utafiti wa kutosha katika Hilo jambo maana hakuna maelezo yanayoweza kumwelezea kwa undani na akalielewa Hilo jambo

3. Tamaa,

Watanzania wengi Wana tamaa ya kufanikiwa haraka kiasi kwamba akiingia katika fursa Fulani asipoona matunda ya kile alichotarajia tayari anaanza kuimba sizitaki mbichi hizi na huku akiishia kusema ni utapeli

4. Kuamini katika nguvu na sio akili

Tulipokuwa shuleni tulijifunza aina za kazi kuwa Kuna zile zinazotumia akili na zile ambazo mtu hutumia nguvu lakini zote hizi ni kazi kikubwa ni kuchagua ww uwe upande gani kulingana na matunda unayoyapata au kutarajia kuyapata

So leo nimekuja na mada inayohusu cryptocurrency,metaverse na NFT

.
Tukianza na cryptocurrency
Cryptocurrency ni sarafu za kidigtal ambazo huwezi kuzishika kw mkono au kuziona kwa macho yenyewe utaona digit tu ambazo zimepewa thamani sawa na fedha ya kawaida na cryptocurrency inaweza kupanda au kushuka thamani yake kwa kulingana na supply and demand ya hio coin yaani uhitaji ukiwa mkubwa Basi thamani huongeza na uhitaji ukiwa mdogo Basi thamani hupungua
Cryptocurrency pia hutunzwa katika platform maalumu ambazo ni digital wallets kama vile remitano,block chain, trustwallets n.k na huweza kutumwa au kupokelewa mahali popote pale duniani bila kujari umbali wake na tayari Kuna baadhi ya nchi zimehalalisha matumizi ya sarafu mtandao Kama fedha Halali kwa malipo ya bidhaa mbalimbali yaani unaweZa ingia dukani kununua chumvi na ukalipa kwa cryptocurrency .

METAVERSE
Kama tujuavyo dunia haijasimama bado Inaenda kwa kasi tayari imekuja teknolojia mpya ambayo inaitwa METAVERSE na hili neno limetokana na maneno mawili yaani META lenye maana ya beyond na VERSE lililotokana na neno UNIVERSE na kuleta neno moja ya METAVERSE
Pia sababu ya mmiliki wa kampuni ya Facebook (Facebook, Instagram na WhatsApp ) ameweza kubadili jina la kampuni platform zake kutoka Facebook na kuitwa META kwa sababu dunia saivi inaelekea huko pia tajiri mkubwa dubiani ELON MUSK aliwahi kusema if you died in METAVERSE you died in real-world

Hii ni teknolojia ambayo mtu anaweza kununua kiwanja ,na anaweza kujenga na kupandisha vyumba u kujenga hotel au kwenda kucheza magame na shughuli zingine nyingi lakini katika virtual world
Nitakuja kueleza namna gani mtu anaweza kunufaika na hii kitu hasa kwa sisi watanzania

NFT

hii inaitwa non-fungible token na mtu yeyote anaweza kutengeneza na kumint nft yake na kuiuza kwenye masoko yake Kama opensea au kupitia exchange Kama binance nitakuja kuzichimba kwa undani zaidi hapo baadae
 
Umeelezea vizuri sana mkuu,Now nimeanza kupata ufahamu juu ya hizi mambo [emoji120]
 
Sikukuu zimeisha… coins gani zinaenda kugain momentum tuanze ku hold??
 
Acha utoto Basi pita kimya ,maana nakuona kwenye thread nyingi unaandika hivi huu ni ujinga ,sio lazima ucomment ,tumia akili sio ilimradi wakuone
"Usimjibu mpumbavu sawa sawa na upumbavu wake... "
The bible says!
 
Wakuu naweza fanya registration kwa Sim nakununua coin kwa sm bila ya computer
 
Mimi natumia Ftx na localbitcoins..
Mkuu naomba kujua jambo hili
'kuna bwana mmoja aliwahi kueleza kuhusu localbitcoin na ktk maelezo yake alisema kwamba
WAWEZA WEKEZA 327 ELFU THEN UKAWA UNAVUNA KAMA 5 ELFU KW CKU je hii ni kweri? na kama ni kweri nianzie wapi mchakato huu?
 
Back
Top Bottom