Technolojia na Kiswahili

Mtumiabusara

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2009
Posts
473
Reaction score
40
Jamani tuelimishane neno au jina lolote la kingereza kwa kiswahili. Naanza na haya


  1. Calculator - Kikokotoleo
  2. Tv - Luninga
  3. Photocopy - Kinakilishi
  4. Laptop - compyuta mpakato
  5. Keyboard - Kichapio ?
  6. Printer -
 
Divert call-chepua simu
Loading-inapakia
 
cholestrol-lehemu
photocopy-kinakrishi?
ceiling fan-pangaboi
 
actions menu -- menyu vitendo
32-bit -- biti-32
animation -- uhuishaji
application -- programu - tumizi
binary -- jozi
blind carbon copy (bcc) -- nakala fiche
bookmark -- alamisha (-link --alamisho)
calculator -- kikokotoo
chat -- sogoa (chat group -- kundi sogozi)
configuration -- usanidi
control panel -- paneli thibiti
country code -- msimbo nchi
 

We kweli mtanzania.
 
Nimesoma neno "computer" ikitafsiriwa kama "tarakeshi"/"tarakishi"/"tarakilishi". Je, waswahili hutumia maneno haya kwa kweli?
 
Nimesoma neno "computer" ikitafsiriwa kama "tarakeshi"/"tarakishi"/"tarakilishi". Je, waswahili hutumia maneno haya kwa kweli?

Ni watumiaji wangapi wa kiSwahili walio na kamusi nyumbani/ofisini kwao? Na pia kamusi ya kiSwahili mpya zaidi imetoka lini? (Ile ya TUKI nadhani ina zaidi ya miaka 15 haijazimuliwa).

Ni kweli watumiaji wengi wa kiSwahili (situmii 'Waswahili' kwa sababu jina hilo lina maana zaidi ya moja) hawayatumii maneno mengi tu hasa yale yanayohusiana na sayansi, utabibu, teknolojia n.k.
 

TUKI wamefyatua kamusi mpya ya kiswahili-kiswahil,ninayo na ni nzur,nenda udsm kwenye jengo la TATAKI,duka la machapisho utaipata,inauzwa elfu 15;ila ubungo terminal yauzwa had elfu kumi,
pia wanatarajia kutoa mpya hiv karibuni ya mambo ya electroniki tuuu
 

Kamusi ya Kompyuta imeshatoka tayari, na ile ya Kiswahili Sanifu sio mpya, ni toleo la 2004..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…