Tegemea haya unapoacha pombe, bangi au sigara, kimoja kitakurudisha uanze upya, kingine kitakufanya uache kuwa mraibu na kuanza maisha mapya

Tegemea haya unapoacha pombe, bangi au sigara, kimoja kitakurudisha uanze upya, kingine kitakufanya uache kuwa mraibu na kuanza maisha mapya

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Kwa kuanza niseme tu kwamba kama vilevi hivyo havikuathiri kimaendeleo basi we endelea tu kuselebuka, Wapo watu kama kina snoop dog wanavuta bangi kwa muda mrefu na maisha yao wala hayana shida zaidi ya kutoboa zaidi.

Maada hii ni kwa wale ambao wanataka kubadili maisha yao na kuona wazi kwamba vilevi hivi vinawawekea vikwazo katika maendeleo yao kiuchumi, kijamii, kiafya, kisaikolojia, n.k. wanatamani kuacha lakini uraibu umewakamata sana.

Hali ya kwanza unapojaribu kuacha vilevi hivi ni kwamba unaacha lakini huna kingine cha kufanya na unaendelea kushinda na marafiki wale wale wa viti virefu, kublaze bangi viwanjani, n.k., kiufupi unakuwa hujabadilika ila ni kwamba umeacha kutumia kilevi, Matokeo yake hapa ni kwamba utaboreka sana, marafiki zako na mazingira yale yale yatakuzonga na mwisho wa siku utarudi tu kuanza upya ulevi wako tena kwa speed ya 4g yenye ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. Wengi wakijaribu kuacha huwa wanapita njia hii.

Hali ya pili unapojaribu kuacha vilevi hivi ni kwamba inabidi utafute mbadala wa kitu cha kufidia mda wa ulevi, kuadili circle ya marafiki, mazingira na hali uliyokuwa nayo unapotumia kilevi. Hapa unaweza kujiwekea malengo mapya kama kupiga mazoezi, kujifunza vitu vipya, kuweka malengo mapya, kufungua biashara za ziada za kwenda kushindia ukitoka kazini, kujiunga na vikundi vipya kama vya wasoma vitabu, kwaya, kucheza draft, n.k. kwa kampani mpya. inabidi uanze kujichukulia majukumu mapya yeye tijamaishani mwako, hali hii inakusaidia kubadili mazingira, marafiki na kujua kwa kuipatia furaha mpya katika maisha yako mapya,

Kupitia mbinu ya pili baada ya muda utajikuta umeanza kupata mabadiliko positive makubwa sana, hautakuwa tena mtumwa wa kujihisi mpweke usipokuwa na marafiki walevi, hautakuwa mtumwa wa kuipata furaha yako kwenye vilevi pekee, vilevi hivi unaweza kujikuta unaviacha kabisa moja kwa moja ama kupunguza matumizi yake katika viwango ambavyo hukuwahi kuja kudhani utaweza na hatimae kuacha kabisa,
 
Pombe nakunywa lakini haijawahi kuniathiri kivyovyote vile kuanzia kiuchumi mpka kiakili...ila kuna kitu inaitwa punyeto acha kabisa niliambiwa ukioa utaacha hiyo kitu lakini pamoja nakuoa bado naendelea kuicharaza.
Nyeto ngumu sana kuachana nayo....inahitaji maombi na maombezi ndo uache. Hivi hivi utakua unaahirisha kwa muda tu sio kuacha kabisa
 
Pombe nakunywa lakini haijawahi kuniathiri kivyovyote vile kuanzia kiuchumi mpka kiakili...ila kuna kitu inaitwa punyeto acha kabisa niliambiwa ukioa utaacha hiyo kitu lakini pamoja nakuoa bado naendelea kuicharaza.
Niliwahi kumsikia jamaa anasema punyeto ni kitu huwezi kuacha,
Ikabidi nimuulize, kwani hujaoa au huna demu?

Akajibu kaka wewe huijui punyeto, huwa napewa mzigo na wife vizuri tu lakini nikiingia bafuni lazima nikashtue kimoja.

Nilishangaa sana, nikiamini huenda ni roho ya shetani na si kawaida
 
Back
Top Bottom