Tegemea kumsikia Nuh Mziwanda kama gospel singer siku za mbeleni

brigedia mafia

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2016
Posts
2,260
Reaction score
2,279
Hitmaker wa ngoma ya Jikeshupa Nuh Mziwanda amebonga na kipaza cha Perfect255 kuhusiana na mipango yake ya baadae kuja kubadilisha aina ya uimbaji na kuwa anaimba muziki wa dini.

Nuh ameiambia Perfect255 kuwa mama yake anapenda sana kumuona anaachana na muziki wa kidunia na kufanya muziki kwa kumsifu mungu kwasababu hata yeye pia ni muimba kwaya.

Nuh anadai kuwa kuna ndugu yake ambae alikuwa akifanya muziki muziki hapo awali lakini alikatazwa kabisa na mama ake huyo, lakini kwa upande wake yeye ilikuwa ngumu kuacha kwasababu alikuwa mgumu kuelewa hadi mwisho wa siku mama yake ikambidi akubaliane na hali.

“Kaka angu alikatazwa muziki na Mama, na kwasasa yuko na mitikasi mingine, ila mimi ni mtu ambaye nimekuwa mbishi kwasababu nimeona ni kitu ambacho nakipenda kupita kiasi. Ombi kubwa la mama hata siku ambazo huwa nikienda nyumbani ni kwamba huwa ananiomba sana niweze kubadilika kwasababu hata yeye ni muimbaji kwaya.” Alisema Nuh mziwanda huku akidai huenda siku moja atabadilika ili kumridhisha Mama yake.
 
Asee nadhan ataimba kaswida
Ebu rekebisha kdogo
Hapana hiyo nimeichukua kama ilivyo si unaona nimechukua screen shot, so sijasema mm haya maneno kasema Nuh mwenyewe , ipitie tena vizuri utaona kasema anaenda kuimba kwaya hajasema kaswida
 
Hapana hiyo nimeichukua kama ilivyo si unaona nimechukua screen shot, so sijasema mm haya maneno kasema Nuh mwenyewe , ipitie tena vizuri utaona kasema anaenda kuimba kwaya hajasema kaswida
[emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87]

[emoji125]
 
Kwenye UISLAMU hakuna kitu kinaitwa kaswida wandugu.
Ni ukosefu wa elimu tu ndio unaowasumbua.
Muziki na vikaragosi vyake haviruhusiwi katika UISLAMU.
Ni vitu ambavyo watu wamejitungia ili kukidhi matakwa ya nafsi zao tu.
 
Duuh!!
Sasa kaswida ni za wapi mkuu!!?
 
Nuhu tangu lini kawa

Nuhu ni Mkristo na sio Mwislamu labda kama amesilimu!!!
 
Nuhu tangu lini kawa

Nuhu ni Mkristo na sio Mwislamu labda kama amesilimu!!!
Sema wewe mkuu, maana nashangaa humu watu walivyo shika bango kudai Nuh ni muislamu ,sijui hicho kibalaghashia hapo juu kina wadanganya?
 
Nuhu hajawahi kuwa muislamu naijua familia yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…