Tegua Haya Mabomu Saba!

Tegua Haya Mabomu Saba!

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Kuna watu umewaruhusu wawe sehemu ya maisha yako kukupotezea muda tu. Haya ni mabomu! Yamelipua uchumi wako, mapenzi yako, siasa zako, kazi yako, dini yako. Huna hamu ya kuishi!

Kuna watu unasema ni watu wako lakini hawajawahi kukupa hela,wala hawajawahi kukupa mchongo wa hela, hata ukipata shida ukiwafuata siku zote hawana msaada.

Yaani hawajawahi kukupa ushauri wowote wa kimaisha, hawajawahi kununua kitu kwako, hawajawahi kukutambulisha kwa mtu yoyote wa maana zaidi ya kukusema vibaya na kukuharibia:kwa watu wa maana wakuone mtu bila maana!

Hawajawahi kukutia moyo katika jambo lolote zaidi ya kukatisha tamaa. Hawa ni mabomu. Wanakupa changamoto za kimatumizi badala ya changamoto za kiutafutaji!

Saa ya kuyategua mabomu haya imefika. Uzuri yako ndani ya uwezo wako. Yategua!

Bomu la Kwanza: Waogopa Hoja

Bomu hili linajumuisha watu wanaoshambulia utu wako badala ya hoja unazozitoa.

Ukihoji jambo utasikia... We situnakujua? Sasa na wewe utatuambia nini!

Utasikia ....nilikuwa nakuamini sana; profesa mzima unakuwa hivyo...

Sasa mimi kuhoji wizi wako vinahusiana vipi na uprofesa wangu?

Watu wa namna hiyo wakianza kuongea tu ondoka zako, na kama ni kwenye simu kata simu, kama ni kwenye whatsapp group usijibu.

Ukijibu wataishia kushambulia utu wako maana hoja hawana. Watakutangaza hadi mlivyokuwa mnashinda njaa utotoni na wakati mambo yanabadilika.

Hata Yesu walisema ni mtoto wa Fundi Selemala wakamua😄😄! Waliongozwa na historia ya umaskini wa familia ya Yesu badala ya kuongozwa na uwezo mkubwa aliokuwa nao.

Watu wanaoshughulika na historia mbaya ya mtu na wakati mambo yanabadilika ni mabomu hatari. Yategue kabla hayakulipukia.

Kama ni honey wako mkipishana kidogo tu anakushambulia kwa kurejea makosa yote ya nyuma hata kama mliishayamaliza mlipue. Huyo ni bomu!

Bomu la Pili: Wakosoaji Watukanaji!

Bomu hili linajumuisha wale watu wanaokukosoa kila unachokifanya kwa lengo la kukudidimiza badala ya kukuinua.

Anayekukosoa ili kukuinua ataanza na kukusifia na baada ya hapo atakupa na mbadala. Hatukani wala kubeza.

Kila binadamu anahitaji sifa njema. Sifa njema ni hamasa ya kutenda zaidi. Asiyekusifia mlipue. Huyo ni bomu!

Majitu ya namna hii hayaonagi mema ya mtu labda mpaka afe! Hata ufanye vizuri kivipi yatakuponda tu. Hata ukiyaangalia yamekaa kishari shari tu. Yanavunjaga moyo majitu haya😀😀😀. Ohoo!

Usijaribu hata kuyaomba ushauri kama unajipenda. Utakata tamaa. Utasikia _ Hauwezi kufanikiwa. Wengi wameshindwa utakuwa wewe?_

Haya mabomu hayaonagi juhudi za watu. Yanaonaga udhaifu tu!

Kuna bomu moja baada ya kusoma makala yangu ya Karagwe Empire lilisema hii makala imejaa makosa mengi. Nilipoliomba linitajie hayo makosa nisahihishe, likanipotea mpaka leo.

Sasa unadhani nia ya hilo bomu ilikuwa nini? Ningelisikiliza na kulitilia maanani ile makala ningeogopa kuisambaza duniani.

Mabomu ya namna hii yamewavunja mioyo watu wengi wakashindwa kuthubutu.

Ndiyo maana huwa nawaambia watu, ukifanya jambo, watu tisa wakafurahi, mmoja akaponda, gonga cheers kwa ushindi halafu songa mbele kwa madaha, mbwembwe na maringo!

Sasa kuna mtu anakatishwa tamaa na mtu mmoja, anakufa moyo na kurudi nyuma na wakati watu tisa walikuwa nyuma yake. Anapondwa Mungu sembuse wewe Heneriko? We vepee😄😄!

Mwingine utamsikia umeona mwanaume wake? Kwakweli kama kuolewa ndo huko oleweni tu!

Utasikia yule dada ni mzuri tatizo miguu.😄😄😄. Sasa miguu inaingiaje hapo kwa kipenda roho kinachokula nyama mbichi? Unadharau miguu na wakati ndiyo imebeba nyama?

Utasikia, Shoga mmejenga nyumba nzuri tatizo madirisha ni madogo. Muulize kwahiyo tubomoe? Bure kabisa!

Bomu la Tatu: Wajuaji Pasipokujua

Hawa wanapenda kusikia ukweli lakini siyo kuambiwa ukweli. Ukiwaambia ukweli mtagombana. Wao wanajua kila kitu. Akina know it all.

Wanapenda kukutawala na kutaka ufanye wao wanavyotaka na hawahitaji kurekebishwa au kukosolewa.

Wanaamini wao ni bora kuliko watu wote. Ndiyo wale wakiendesha gari kila dereva anayewapita lazima wamtukane kwamba anaendesha vibaya!

Akipita boda wanatukana. Akikatiza mwenda kwa mguu wanatukana. Hata wakikutana na ng'ombe barabarani wanatukana ng'ombe mpaka mswaga ng'ombe.

Yaani safari nzima ni yeye na matukano. Huu ni ugonjwa pia! Magonjwa yako mengi!😀😀🫲🫲. Ukiishaona watu wote ni wajinga basi wewe ndo mjinga.

Bomu la Nne: Akina Sina Wivu Ila Roho Inauma!

Kwakweli hawa niseme tu ni watu wenye roho mbaya. Huamini kuwa kila kitu kizuri kinatakiwa kitokee kwao tu. Ukipata wananuna, ukikosa wanatabasamu.

Wao hata wasikie jambo zuri au kubwa kiasi gani la mtu mwingine wao hujifanya kuliona kama la kawaida tu.

Utasikia mbona wapo wengi waliofikia hapo”, “mambo ya kupita hayo, cha muhimu uzima bwana”, “mafanikio ya watu hayanihusu bwana”.😄😄😄. Lipua haraka hili bomu. Lipuaaa!

*Bomu la Tano: Akina Changu Changu Chako Chetu"

Hawa ukiwa na hela wanakuwa rafiki zako, ukiishiwa wanaishia. Wanataka kufaidika na vyako huku vya kwao huvioni.

Wanajijali wao tu, na hawawajali wengine. Wanaangalia kitu kitakachowanufaisha wao tu bila kuangalia kama kina madhara kwa wengine.

Watu kama hawa wanapenda kupokea tu, hawapendi kutoa. Siku zote hawana hela. Hata mkitoka out mkaagiza, bili ikija wanajifanya kwenda kupokea simu. Wanarudi bili imelipwa. Hawa ni mabomu. Lipua!

Bomu la Sita: Akina Hasira za Mukizi

Hawa watu jambo dogo tu wanawaka na kuzira. Hawa ni kama jongoo. Ukimgusa amejikunja.

Ukiwa nao utapoteza muda kuwabembeleza na wakati dunia hii siyo ya kubembeleza mtu. Akisusa we kula, sepa!

Lakini pia hawachelewi kuanzisha ugomvi. Watakuingiza pabaya. Hawa ikiwezekana walipue hata leo! Najua kuna mmoja uko naye hapo anakuchosha tu.

Bomu la Saba: Walioumizwa Bila Kupona!

Hili ni kundi la watu walioumizwa na mapenzi, umaskini, manyanyaso, ajira na mioyo yao bado haijapona vizuri. Hawa mazungumzo yao yamejaa vitisho. Ukiwasikiliza sana hutafanya kitu.

Mwanamke aliyeumizwa na mapenzi atakwambia wanaume wote ni kenge tu kwa sababu tu mwanaume wake alikuwa kenge akamgonga.

Mwanaume aliyepigwa tukio atakwambia siku hizi hakuna wanawake wa kuoa, wote ni washenzi tu kwa sababu mwanamke wake alikuwa mshenzi.

Aliyeumizwa na mikopo atakwambia mikopo ni sumu kwa sababu yeye alifanya biashara kwa mkopo bila kujipanga akafilisika!

Aliyefukuzwa kazi atakwambia siku hizi hakuna kazi za maana kwa sababu amesoma vizuri akakosa kazi ya maana.

Aliyeumizwa na umaskini akapata maisha ya kubadilisha mboga huamini watu waliomzunguka wanamchukia na kumuonea wivu kwa sababu amewazidi😀😀

Hata tembea yake ni kama mtu aliyetoka kucheza mpira, amechoka, anaswaga za kilemavu fulani hivi. Anaamini ameshayamaliza maisha. Mliobaki mnacheza tu.

Hawa wanatabia kama za mtoto wa mwisho aliyekulia kwenye umaskini akapata ahueni. Atawadharau wakubwa zake kwamba ni wavivu. Haya ni madhara ya kukosa lishe bora utotoni, inaathiri mpaka ukubwani.

Kama una mtu wa namna hii, huyo ni bomu, lipua!

Denis Mpagaze
________________
 
Wakati nalipua mabomu haya nijiite sajenti au bregedia?
 
Back
Top Bottom