TEHAMA NA TANZANIA YA KESHO:
Teknolojia ni elimu ya utengenezaji, utumiaji wa vifaa vya maarifa, mashine, mifumo au njia zitumikazo kutatua tatizo kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa jambo Fulani katika jamii. TEHAMA ni kirefu cha technolojia ya habari na mawasiliano, inajumuisha vifaa mbalimblai vya kiteknolojia ambavyo vinatumika katika kutengeneza, kuhifadhi na kusambaza taarifa mbalimbali.
Katika maendeleo ya taifa lolote ulimwenguni TEHAMA ina mchango mkubwa sana katika kukuza uchumi pamoja na kupandisha thamani ya bidhaa mbalimbali. Kwa kiwango Fulani taifa letu chini ya uongozi na serikali ya Dr. Samia Suluhu Hassan limeanza kupiga hatua katika ukuaji na uendelezaji wa TEHAMA nchini kwa manufaa ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa Tanzania ya leo na kesho.
Licha ya hatua kadhaa ambazo serikali yetuinazichukua kuhakikisha TEHAMA inakua nchini lakini bado kuna changamoto ambazo zinarudisha nyuma maendeleo ya TEHAMA. Kwa ukuaji wa Teknolojia ya habari na mawasiliano nchini kuna mambo kadhaa ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi ili kukuza na kuendeleza TEHAMA nchini, kwa kipindi cha miaka mitano ijayo mambo yafuatayo yakifanyiwa kazi na serikali pamoja na watanzania kwa ujumla yatapelekea Tanzania ya kesho kuwa imara sana katika suala zima la maendeleo kwa sababu TEHAMA inamchango mkubwa sana katika kuleta maendeleo ya taifa na kwa mtu mmoja mmoja. Mambo hayo ni,
Kuandaa mazingira rafiki kwa wawekezaji kutoka nje; Ili kuweza kuimarisha ukuaji wa TEHAMA nchini serikali inapaswa kuandaa na kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa wawekezaji kutoka nje ili waweze kupata nafasi ya kuwekeza nchini, hii itasaidia katika upanuaji wa technolojia ya habari na mawasiliano huku ikichangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa maendeleo ya taifa na kuongeza fursa za ajila kwa wananchi hususani vijana.
Mazingira mazuri kwa wawekezaji yataleta idadi kubwa ya wawekezaji waatakaohitaji kuwekeza nchini. Mfano uwekezaji katika vituo vya redio na runinga, uwekezaji katika taasisi za elimu kama vyuo vya kati na vyuo vikuu vitakavyokuwa vinatoa wataalamu wengi wa TEHAMA nchini, makampuni ya kusamabaza na kutoa huduma za kimtandao kwa watanzania kwa gharama nafuu.
Kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi na umuhimu wa TEHAMA kwa taifa na jamii; Serikali inapaswa kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu ya TEHAMA kwa wananchi juu ya umuhimu wake na matumizi sahihi ya TEHAMA lkwa maendeleo ya taifa kwa ujumla. Licha ya hatua ambazo Tanzania kama taifa imepiga hadi sasa katika sekta ya technolojia ya habari na mawasiliano lakini bado idadi kubwa ya wananchi bado hawana ueleewa wa kutosha juu ya TEHAMA, bado hawana elimu ya kutosha juu ya matumizi sahihi ya TEHAMA, bado idadi ya wataalamu wa TEHAMA nchini ni ndogo ukilinganisha na mahitaji ya jamii. Kwa mfano kuna baadhi ya sehemu nchini utakuta halmashauri nzima ina mtaalamu mmoja wa TEHAMA anayeshughulikia masuala yote ndani ya halmashauri, hivyo Serikali kwa kipindi cha miaka mitano ijayo inapaswa kuongeza idadi ya wataalamu ikiwa ni kuwahamasisha pia wananchi hususani vijana kuwa na ari ya kusomea TEHAMA, pia itaondoa tatizo la upungufu wa wataalamu na kuifanya jamii ya Watanzania kuelewa umuhimu wa TEHAMA kwa amaendeleo ya taifa la kesho.
Kuongeza idadi ya watumiaji na wamiliki wa vifaa vya TEHAMA kwa watanzania waishio mijini na vijijini; Serikali inapaswa kuongeza idadi ya watanzania wanaomiliki na kutimia vifaa vya TEHAMA katika maeneo yote ya mijini na maeneo ya vijijini. Licha ya jitihada za serikali kuhakikisha nishati ya umeme inakuwa ya uhakika katika maeneo yote nchini lakini bado utumiaji na umiliki wa vifaa vya kisasa vya TEHAMA kwa watanzania waishio vijijini bado ni changamoto, vifaa kama simu janja pamoja komputa mpakato au kishikwambi kwa watanzania wengi waishio vijijini ni changamoto wengi wakitaja sababu ni gharama kubwa ya upatikanaji wa vifaa hivyo. Ukilinganisha na sera ya taifa ya TEHAMA ya mwaka 2013 serikali ilikuwa na lengo la kuongeza idadi ya watumiaji na wamiliki wa vifaa vya mawasiliano lakini hadi sasa kiwango bado si kile ambacho kilikusudiwa kufikiwa. Kuelekea miaka mitano mbele serikali ili kutimiza lengo ni vyema kama itachukua hatua za kupunguza kiwango cha kodi kwa vifaa vyote vya mawasiliano hii itapunguza bei ya vifaa hivi sokoni na itamshawishi hata mtanzania wa kipato cha chini aweze kumudu gharama zake.
Serikali kuunga mkono jitihada za vijana wa kitanzania wanaowekeza katika sekta hii kwa kuwapatia mitaji na elimu ya uwekezaji wenye tija; wapo vijana na watanzania mbalimbali wanaotamani kuona Tanzania ya kesho inapiga hatua kubwa sana katika sekta ya Technolojia ya habari na mawasiliano kwa kuanzisha vituo vyao mbalimbali ili kuendeleza ukuaji ya TEHAMA nchini lakini vijana wengi wanashindwa kufikia malengo kutokana na ukosefu wa mitaji ya kutosha katika kutimiza malengo yao. Ili kuwasaidia vijana hawa Serikali inaombwa kuwawezesha kwa elimu, mitaji na mazingira mazuri kwa ajili ya kuendeleza mipango yao kwa ajili ya ukuaji wa maendeleo kwa Tanzania ya sasa na ya kesho. Vijana wanaoanzisha vituo vidogo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya TEHAMA pamoja na huduma mbalimbali za kimtandano kwa wananchi watiwe nguvu kwa kupatiwa mitaji na elimu Zaidi hii italisaidia taifa kukuza maendeleo kupitia TEHAMA.
Serikali kuhamasisha wanawake kujihusisha na elimu ya Teknolojia ya habari na mawasiliano; Bado idadi ya wanawake nchini wanaojihusisha na sekta hii bado ni ndogo ukilinganisha na idadi ya wanaume, serikali inapaswa kuweka jitihada kubwa ili kuliiunua kundi la wanawake kama ambavyo inajitahidi katika sekta zingine ili kukuza kiwango cha TEHAMA nchini. Elimu Zaidi kwa wanawake itolewe ikiwa ni pamoja na uwezeshjwaji kwa makundi ya akina mamam na vijana wa kike ili nao waweze kuwa mstari wa mbele katika maendeleleo ya TEHAMA ikiwa ni pamoja na kupata wataalamu wa TEHAMA wanawake.
Serikali ikifanyia kazi mambo machache yaliyoainishwa hapo juu, tutarajie kuiona Tanzania mpya katika ulimwengu wa TEHAMA kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Upvote
6