Tekno: Diva wewe ni msichana mrembo, kwanini huna mpenzi?

DivaDaily

Member
Joined
Oct 2, 2015
Posts
18
Reaction score
15
Siku za hivi karibuni mtangazaji huyo maarufu amekuwa akihoji wasanii wengi wa nje ya Tanzania wakiwemo Iyanya, Patoranking, Maurice Kirya na sasa amezungumza na hitmaker wa Duro, Tekno Miles wa Nigeria.

Kwenye mahojiano hayo Diva amemuuliza staa huyo kuhusu issue za muziki na ofcource kuhusu malavidavi. Hata hivyo kabla ya kujibu swali, Tekno aliamua kugeuka mtangazaji kwa muda na kumbananisha Diva kuhusu maisha yake ya mahaba.

“Do you have a boyfriend,” alihoji muimbaji na producer huyo wa Nigeria. “No, I am not dating, I don’t have a boyfriend,” alijibu Diva.

“Why? You are very hot, you should have a boyfriend,” alichombeza Tekno.

“I am hot?” Diva aliuliza kana kwamba masikio yake yamemdanganya kwa kile alichosikia.

“Yes, I see a lot of fans love you in Tanzania, you should be taken right now,” aliongeza Tekno.

Diva alijibu kuwa kwa sasa anapenda kuwekeza akili na nguvu yake kwenye kazi yake zaidi. “I don’t have a boyfriend, very serious, I am just single, I am busy working,” alisisitiza.

Hata hivyo kwa upande wake Tekno kama ilivyo kawaida kwa wasanii wengi maarufu, alisema hana mrembo yoyote na kueleza kuwa ‘I am in love with my music.’

Hata hivyo alikiri kuwa wanawake wengi wanamtaka wavunje naye amri ya sita japo amekuwa akiwachomolea bila huruma!

 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1443785276.593922.jpg
    29.3 KB · Views: 316
  • ImageUploadedByJamiiForums1443785296.417278.jpg
    61.8 KB · Views: 263
  • ImageUploadedByJamiiForums1443787939.926031.jpg
    26.8 KB · Views: 1,377
Diva unajitekenya na kucheka mwenyewe, unajifungulia uzi but who care abt ujinga wako?
 
Hii id inaendana na anayeongelewa imevamia humu

Ukileta uzi mwingine mwaga cv yako labda utajulikana wewe nani
 
Huyu binti nasikia ni mtoto wa rahisi wa tiefuefu. Sijui huwa ni kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…