JamiiCheck
Member
- Nov 3, 2023
- 98
- 122
Matamshi ya chuki, propaganda za kisiasa na uongo si matatizo mapya mtandaoni, nyakati za uchaguzi kama hizi huzidisha zaidi matatizo hayo. Matumizi ya roboti, au akaunti bandia (Feki) za mitandao ya kijamii, imerahisisha zaidi kueneza habari zisizo sahihi kimakusudi, pamoja na uvumi usio sahihi au aina nyinginezo za upotoshaji.
Lakini roboti zilizoathiri misimu iliyopita ya upigaji kura mara nyingi zilitoa sentensi ambazo hazijaundwa vizuri, zisizo sahihi kisarufi. Kadiri miundo mikubwa ya lugha (mifumo ya kijasusi bandia inayounda maandishi) inavyozidi kufikiwa na watu wengi zaidi, watafiti wengine wanahofia kuwa akaunti bandia za mitandao ya kijamii zitaboresha zaidi uandishi wake hivi karibuni.
Kampeni za upotoshaji wa taarifa zimeandaliwa kuongeza matumizi ya Akili Mnemba ili kuchochea uongo wa uchaguzi, kulingana na utafiti mpya uliochapishwa na PNAS Nexus.
Katika hilo, watafiti wanakadiria kwamba, kulingana na “tafiti za awali za mtandao na mashambulizi ya kiotomatiki ya algorithm”—Akili Mnemba itasaidia kueneza maudhui yenye chuki kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii karibu kila siku mwaka wa 2024. Mapungufu yanayoweza kutokea, waandishi wa utafiti wanasema, yanaweza kuathiri matokeo ya uchaguzi katika nchi zaidi ya 50 zinazofanya uchaguzi mwaka huu, kutoka India hadi Marekani (Tanzania ikiwemo).
Majukwaa madogo ya kimtandao yameunganishwa vizuri na ikiwa maudhui potofu yatatoka kwenye mitandao hii hadi kwenye tovuti kuu za kijamii kama vile YouTube, watafiti wanakadiria kuwa watu bilioni moja wanaweza kuathiriwa nayo.
Uchunguzi wa habari potofu katika chaguzi zilizopita umebainisha jinsi roboti kwa ujumla zinavyoweza kueneza maudhui hasidi kwenye mitandao ya kijamii, hivyo basi kuchezea mijadala ya mtandaoni na kuondoa uaminifu. Zamani roboti zingechukua ujumbe ulioundwa na mtu au programu na kuzirudia, lakini miundo mikubwa ya lugha ya leo (LLMs) inaboresha roboti hizo kwa kipengele kipya: maandishi yaliyoandikwa na mashine ambayo yanafanana na kusikika kuwa ya kibinadamu.
Wataalamu wanatabiri kuwa habari za uongo zinazotokana na Akili Mnemba zitaenea kwa upana zaidi wakati huu wakati mataita zaidi ya 50 yakifanya chaguzi zao hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini na taarifa wanazoona kwenye mitandao ya kijamii, na wanapaswa kuzihakiki kabla ya kuziamini.
Kufikia Jukwaa la JamiiCheck, bofya HAPA.