Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Umiliki wa teknolojia za mawasiliano ni jambo muhimu katika kuitawala dunia. Hiyo imeonekana kwa tajiri mkubwa wa dunia Ellon Musk anayemiliki satelite ya Starlink.
Wakati vita kati ya Ukraine na Urusi vikianza jeshi la Urusi liliwahi kuibomoa minara ya mawasiliano ya makampuni ya simu ili kuinyima Ukraine miundombinu ya mawasiliano.
Kwa vile Ukraine ilikuwa imelihisi hilo kutokea ilikuwa imeshaingia mkataba na Ellon Musk ili waweze kutumia mtandao wake wa mawasiliano kupitia satelite ya starlink.Hilo limelsaidia jeshi la Ukraine kuweza kuwasiliana bila kuzuiwa wala kudukuliwa na Urusi.
Kwa upande wake Urusi ilipoona hivyo ikatoa vitisho kwa Ellon Musk kuhusiana na kifaa chake hicho kilichoonekana kuipa nguvu Ukraine.
Kuona hivyo Ellon ikabidi awakabili waUkraine kwamba wakubali kuaachia maeneo yaliyotekwa na Urusi Ukweli ambalo hata Umoja wa mataifa haujauzingatia ili kumaliza vita. Kwa upande wa Taiwan amewataka waache kushirikiana na Marekani katika kuichokoza China ili kuepusha vita visivyokuwa na haja.
Akisimulia maandamano ya Iran kupinga hijabu,Ellon Musk na teknolojia zake inaonekana wamehusika katika kuitingisha Iran.
Anasema watu wa Iran walimuomba watumie mawasiliano yake na alipowakubalia wameweza kuwasilaiana na kuchocheana bila kizuizi.
Hiyo imeonesha kuwa tatizo la Iran wala si hijabu tu isipokuwa ni nguvu ya teknolojia katika kuwaamulia watu cha kufanya na matumizi yake mabaya kwa watu wenyewe.
Wakati akizungumza na wafuatiliaji wake wa twitter wanaofikia milioni 108 baada ya kauli ya Biden kuhusu hofu ya kutokea vita vya nyuklia, Ellon Musk amesema siku hizi hapati usingizi akifikiria namna gani ya kumaliza vita hivi kabla havijavuka mpaka na kuwa vita kamili ya dunia itakayohusisha matumizi ya nyuklia.Kauli kama hiyo haijasikiika kutoka kwa katibu mkuu wa UN.