Teknolojia inatuletea yaleyale ya kwetu yaliyotiwa nakshi ya udigitali

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Zamani kule vijijini tulizoea kuweka pazia au milango ya mguu pande mguu sawa na hakuna mwizi aliyethubutu kuvunja! Na aliyethubutu kufanya hivyo cha moto kilimpata.

Hii haina tofauti na sasa, teknolojia imekuja na milango ya vioo! Ni yale yale kama yetu lakini huku yamekuja kwa sura ya kioo.

Kule kijijini kuliwa na mageti ya miti au magogo lakini sasa teknolojia imekuja na mageti ya access control yaani unakuta kifimbo tu kimeziba njia kama pale airport au Milimani City ili uingie lazima eti uchomeke kadi! Hii ni mbinu ileile katika sura udigitali.

Niliwahi kwenda Tanga nikasahau kuwasalimia wazee wa mji kabla ya kukaa! Niliponyanyuka suruali ilikuwa imeliwa na mchwa matakoni, hii ilimaanisha kuwepo kwa adabu! Ilitakiwa nisalimie kabla ya kukaa.

Kama hii haitoshi, zamani huko kijijini waliweza kuhifadhi nyama au maziwa kwa mda mrefu pasipo kuharibika, hii sasa pamoja na kuwepo friji bado vitu vinaharibika.

Zamani mtu aliweza kuwa na ng'ombe elfu 2000 lakini akipotea mmoja tu lazima ajue, na akimtafta hata amkute kwenye kundi anaweza kumchambua! Hivi sasa tuko na DNA ni yaleyale ya uzamani kuwekwa katika sura ya udigitali.

Ushauri wangu kama huna pesa ni vyema ukajifunza njia za asili ili kupata kitu kilekile kwa gharama nafuu.
 
Hata leo watu kundi wanaweza kusafiri kwenye flat round basket yenye diameter ya 60cm bila fuel tanks wakafika salama
 
Back
Top Bottom