SoC02 Teknolojia inayoweza kutatua matatizo mbalimbali Tanzania

SoC02 Teknolojia inayoweza kutatua matatizo mbalimbali Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Man Chussey

Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
5
Reaction score
1
1.0 UTANGULIZI

Teknolojia ni suluhisho inayotokana na matumizi ya akili ya mwanadamu baada ya kufanya tafiti au hutokea kwa dharura. Teknolojia inalenga kurahisisha au kutatua changamoto fulani iliyopo katika jamii husika. Teknolojia fulani inaweza kuwa katika taifa moja au taifa moja na lingine/mengine.

Teknolojia inakuwa kwa kasi sana zaidi ya vile ambavyo tunavyofikiria. Taifa kama taifa linapaswa kuwa na mikakati maalum ya kuhakikisha mazingira mazuri ya teknolojia yanakuwepo.

Teknolojia hutokana na matumizi ya akili ya mwanadamu na huwa ni maalum kwa kurahisisha au kutatua changamoto fulani iliyopo eneo husika. Mfano matumizi ya mifumo ya Tehama.


2.0 IPI HALI YA UKUAJI WA TEKNOLOJIA TANZANIA?

Mazingira ya ukuaji wa teknolojia nchini Tanzania sio mazuri sana kwani watu wengi wamekuwa wakionesha ubunifu wao lakini wanapata ushirikiano mdogo sana kutoka serikalini, na hali hiyo kupelekea ubunifu wao kushindwa na kubakia kwenye makaratasi. Lakini bado ushiriki wa serikali sio mzuri ata kwenye teknolojia zilizoanza kujikongoja, mfano mfumo wa NALA (applikesheni ya kutuma pesa mataifa mengine) umebuniwa na mtanzania lakini unafanya kazi vizuri zaidi nchini Kenya, Rwanda n.k.

Kitu kingine ni kodi ya mapato kuwa kubwa sana ambapo hupelekea biashara au kampuni nyingi kushindwa kupata faida/pesa ya kuendeshea shughuli zote.


3.0 KWANINI TANZANIA TUNAHITAJI TEKNOLOJIA YETU?

Dunia ikiwemo na Tanzania inahitaji teknolojia kwaajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazokumba sekta mbalimbali kama za kiuchumi, afya, elimu, kilimo, maji, hali ya hewa n.k. Katika taifa la Tanzania kuna kila aina ya changamoto kwenye kila sekta zilizoorodheshwa hapo juu, hivyo kunahitaji la kuwa na teknolojia zetu zitakazo buniwa na watanzania, maalum kwa ajili ya kutatua changamoto zetu katika kila sekta.

Utegemezi wa teknolojia kutoka mataifa mengine unaweza usiwe na manufaa kwa taifa la Tanzania kwa asilimia kubwa kwa sababu teknolojia zile zinaweza kuwa sio mahsusi kwa taifa la Tanzania, kwahiyo zikawa na msaada usioweza kutatua tatizo/changamoto kwa asilimia kubwa zaidi, hivyo tunahitaji teknolojia zetu wenyewe kwa manufaa ya nchi yetu.


4.0 BAADHI YA TEKNOLOJIA TUNAZOHITAJI TANZANIA
  • Teknolojia ya kompyuta #1; teknolojia hii inajumuisha computer science na computer engineering, ambapo kwenye computer science itajikita zaidi katika utengenezaji wa mifumo na programu za kompyuta, na computer engineering itajikita zaidi na utengenezaji, uboreshaji na ufuatiliaji wa vifaa vyote vinavyohusiana na kompyuta. Ulimwengu ujao utakuwa ni wa kidijitali kwa asilimia karibia zote, hivyo hatuna budi kuwekeza nguvu zetu kwenye hili. Kozi hizi ni muhimu sana kufundishwa mashuleni kuanzia ngazi ya awali mpaka kufikia ngazi fulani ya elimu.
  • Teknolojia ya kompyuta #2; kwakuwa kasi ya ufanyaji kazi wa kompyuta zetu za kawaida (Classic Computer) kuwa ndogo na isiyoridhisha, dunia imegeukia kwenye kompyuta mpya zenye kasi kubwa zaidi (Quantum Computer), na tayari baadhi ya makampuni makubwa duniani kama Google yameanza kutengeneza. Msingi wa kompyuta hii unaanzia kwenye Fizikia ya kisasa (Modern Physics – Quantum Physics). Kozi hii pia nimuhimu kufundishwa mashuleni kuanzia ngazi ya awali mpaka ya juu.
index.jpg
PR20210629-0019-01.jpg

Picha ya Quantum Computer kutoka mtandani - Google
  • Teknolojia ya Mashine na Akili za Kubumba (Machine Learning & Artificial Intelligence); ukisikia ulimwengu wa kisasa na automation ndio huu, programu ya kompyuta inasoma taarifa zilizopo na kusema nini kitatokea na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike. Teknolojia hii inakwenda sambamba na matumizi ya kompyuta za kuantam, na kazi nyingi zinazofanywa na watu katika viwanda zitakuwa zikifanywa na mashine na katika ufanisi mkubwa zaidi.
deep.jpg
machine.jpg

Picha kutoka mtandaoni za machine learning, A.I na Deep Learning -Google
  • Teknolojia ya Bayoteknolojia; matumizi ya viumbe hai vidogo zaidi katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kama antibiotics, homoni n.k. Teknolojia hii ni muhimu sana katika ukuaji wa teknolojia ya nchi kwani inakuza sekta ya viwanda.
bio2.png
biotech.jpg

Picha za Bayoteknolojia kutoka mtandaoni - Google

Teknolojia za ziada zinazoweza kutufaa kwa maendeleo ya taifa:-
  • Teknolojia ya anga za mbali; teknolojia inayohusiana na kufanya tafiti za anga za mbali kutafuta maisha nje ya dunia.
space.jpg

Picha kutoka mtandaoni ya teknolojia ya anga - Google
  • Teknolojia ya Virtual Reality; teknolojia inayohusiana na utengenezaji wa ulimwengu wa kidijitali (Digital world) ambapo mwanadam atapata kuona kupitia vifaa maalum na kupata uzoefu Fulani (Digital experience).
virtual.jpg

Picha kutoka mtandaoni ya virtual reality - Google
  • Teknolojia ya kubadilisha jinni (Gene-editing technologyCRISPR); teknolojia yenye kutafuta namna ya kubadili mpangilio wa jinni (genes) ili kupambana na magonjwa mbalimbali ya viumbe hai kama kansa n.k.
GENE.jpg

Picha kutoka mtandaoni ya teknolojia ya kubadili mpangilio wa jini (Gene) - Google
  • Teknolojia ya Human-computer Interface; teknolojia hii inamuwezesha mwanadam aweze kuwasiliana na kompyuta moja kwa moja. Mwanadamu anaweza wekewa kifaa fulani ili aweze kuwasiliana na kompyuta.
human.jpg

Picha kutoka mtandaoni ya mwanadamu akiwasiliana na kompyuta - Google

5.0 NINI KIFANYIKE TUWEZE KUWA NA TEKNOLOJIA ZETU?
  • Kuwekeza katika elimu yenye manufaa; tafiti nyingi zinatakiwa kufanywa katika upatikanaji wa mtaala mpya wa elimu wenye uwezo wa kutufikisha kwenye dunia ya kwanza.
  • Serikali kupeleka wataalamu kwenda kupata uzoefu; angalau watu 20 mpaka 50 wa sekta mbalimbali kila mwaka wakiwa wanapelekwa katika mataifa yaliyoendelea kupata mafunzo na kuona jinsi wanavyofanya kazi, itasaidia ukuaji wa teknolojia yetu hapa nchini.
  • Ushiriki na nchi za jirani za Afrika Mashariki; kwasababu tuna changamoto karibia zote zenye kufanana, ni muhimu kuunganisha nguvu ili tushirikiane katika utengenezaji wa teknolojia ya pamoja kupitia kuanzishwa kwa chombo cha ushirikiano wa teknolojia cha Afrika Mashariki (East Africa Technology Cooperation – EATech Cooperation).
  • Kuanzisha chuo maalum kwa ukuzaji vipaji vya ubunifu wa teknolojia; kupitia shule/chuo hiki, wale wote watakao kuwa na vipaji na teknolojia wamezibuni watapata msaada wa kielimu, kiufundi na kifedha ili kufanya bunifu zao zifanye kazi. Serikali kupitia shule/chuo hiki, inawajibu wakutoa ushirikiano wa asilimia kubwa ili kufanikisha.
6.0 HITIMISHO
Kuwa na teknolojia yetu iliyobuniwa na sisi wenyewe ni muhimu sana kwani tutapunguza asilimia za kupata misaada yenye masharti magumu na tutaweza kutatua changamoto zetu wenyewe. Kila taifa kuendelea, inatokana na ukuaji wa teknolojia zinazobuniwa na wananchi wake.

Hakika tunaweza kama tukiamua na kuthubutu kama mataifa mengine yalivyothubutu. Ni wajibu kwa serikali kuwa sikivu na kufanyia kazi yale yote mazuri wananchi wake wanayoishauri.

Jina: Hussein Juma Jitihadi
Barua pepe: husseinjitihadi@gmail.com
Simu: 0766973326
 
Upvote 1
Shukran, ndugu zangu.... Nawakaribisha kwa mdahalo katika makala hii na naombeni mnipigie kura.
Akhsante.
 
Back
Top Bottom