Teknolojia iwe nyundo yetu

Teknolojia iwe nyundo yetu

Tatu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2006
Posts
1,143
Reaction score
372
Jamii yetu ina changamoto nyingi sana ambazo tunaweza kuzifanyia kazi na kuzipatia ufumbuzi kwa kutumia technology. Tumeshatoka kwenye zama za kutumia nyundo (figuratively) katika kila kitu.

Tukianza kuorodhesha changamoto ambazo jamii yetu inazo, nafikiri zitakuwa ni nyingi sana na wala siku nzima haitoshi kuzimaliza. Kibaya zaidi, unapoongea na watu tofauti kuhusu kutatua hizi changamoto, watakujibu, "Ya nini bwana? Tumeshazoea.

Hakuna jibu au neno ninalolichukia kama, "Nimeshazoea au Tumeshazoea" hasa ikiwa ni shida au changamoto fulani. Hilo neno linaonyesha mtu amefikiwa mwisho wa kufikiri au amekata tamaa. Sio sawa, tuamke.

Technology imesharahisisha mambo mengi sana. Kilichobaki ni jamii yetu kujifunza na kuanza kutatua changamoto tulizonazo. Tumeshatafuniwa kila kitu. Ni sisi tu kuifanyia kazi.
 
Na mimi hivi karibuni nazindua karoboti changu kanaitwa 'chiwema'
 
Na mimi hivi karibuni nazindua karoboti changu kanaitwa 'chiwema'

Hongera ndugu. Kila mtu akichangia kwa uwezo wake na nafasi yake, tutafika mbali. Attitude iwe, "Hata sisi tunaweza."

Hakuna haja ya kutegemea mataifa mengine kwa changamoto zilizo ndani ya uwezo wetu.
 
Ni jambo jema; ndiyo maana tunapaswa kujifunza namna ya kuishika na kuitumia kwa weledi mkubwa.

Kuwa tu na nyundo ndani hakusaidii chochote kama mtu hawezi kuulenga na kuukomea msumari barabara.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom