Teknolojia Mpya kutoka Japan ya kupunguza ulaji wa Mafuta kwenye Gari

Teknolojia Mpya kutoka Japan ya kupunguza ulaji wa Mafuta kwenye Gari

Joined
Feb 4, 2022
Posts
15
Reaction score
17
UTANGULIZI

UWGxAhT2ko9kPqn02JMkp4Ut_tAQZW6XAMNMx23eA-aru0UhpFU4_j14ufH-fb0nd3E5N8AzQgoOmPpK9-fYhKbZOwFMZoDDJe3AUTx2hZdSPXnytmswHYiNnplfps5G8CFnjfA0


Masaaki Imai Mkufunzi wa kijapan wa mifumo ya ubora maarufu kama “kaizen” aliwahi kusema “siku moja isipite bila kuhakikisha kuna mahali umeboresha katika kazi/ chombo chako na maisha yako.Hata kama ni padogo kiasi gani.

⛽ Kwa miaka mingi vyombo vya moto vinavyoingia nchini mwetu kutoka UK na Japan ni “USED” maana yake sio vipya na uimara wake umepungua kiasi, haswa kwenye maeneo ya Engine na Body.

⛽ Ulaji wa wa mafuta katika magari haya huwa tofauti na lilivyokuwa jipya (Brand New). Na sababu kubwa sana inayochangia ulaji wa mafuta kwenye gari ni ufanisi katika mifumo ya hewa na kusababisha kuwa na mlipuko hafifu wa engine *(incomplete combustions).

  • Kumbuka mlipuko wa Engine ndio huipa gari mwendo “energy”.Na mlipuko unapokuwa hafifu ni sawa na kupika chakula na kuni mbichi, utaivisha chakula kwa muda mrefu na moshi utakuwa mwingi sana. Ndivyo ilivyo pia katika gari yako.

🚨 Dalili za incomplete combustions ni pamoja na gari kuwa zito,kutoa moshi wa ukaa,kukosa accelerations nzuri na kula mafuta.

⛽ Mafuta yana gharama kubwa sana kwa mwaka na wengi wetu hatufahamu gharama halisi ya matumizi yetu.

⛽ Hebu fikiria kidogo tu kwamba gari yako inaenda service kila baada ya kilometa 4000 na gari lako lina uwezo wa 1300cc-1500cc na linatumia lita 1 kwa kilometa 12 (12km/litre)


FACTS NI HIZI:

🚥 Baada ya km 3000 utakuwa umetumia wastani wa lita 250 (3000/12)

🚥 Kwa gari hilo hilo ukipata kifaa cha kukuwezesha kufika Km15/Litre utatumia wastani wa lita 200 .(3000/15)

🚥 Ukitoa Lita za awali 250 na lita 200 unapata lita 50 ziada ambazo ni sawa na wastani wa Tsh. 123,700 kwa bei ya mafuta.(Tsh 2,474 kwa petrol)

🚥 Kama unaenda service mara 4 kwa mwaka maana yake unaokoa TZS ngapi? Tsh. 123,700*4= Tsh. 494,800 kwa mwaka.hizi ni sawa na lita 200

🚥 Kwa miaka mitano unaokoa lita ngapi? Kwa miaka 10 ya umiliki wa gari lako je?


TEKNOLOJIA KUTOKA JAPAN

Chuo kikuu cha Tokai University Faculty of Engineering, walifanya utafiti baada ya kugundua magari mengi yanachangia ukaa katika Dunia,na haswa katika nchi zinazoendelea.

Hapo ndipo walipogundua Teknolojia ya AdPower ambayo ni kifaa kinachowekwa katika mfumo wa hewa wa gari ili kufanya mlipuko kamili (100%complete combustions).


U7vDlPnTW4EjiyUwUESB6qjiWG7D4UHUjUh7F85cn7CFBtnW5brOLeTJ5cULiXHOQ__iWoXxqxqf6bHSVu3rDHXUFik1zGC4_z4hUR5PuMVo7WEATjDzS6Kvyi4KLsnh15p8uznY


Kumbuka moshi unaotoka baada ya mlipuko katika engine ni matokeo ya kutokuwa na mlipuko kamili haswa kutokana na uchakavu katika mfumo wa hewa wa gari.Teknolojia hii inaongeza uhai wa engine yako na kusafisha hewa ya ukaa itokayo katika gari yako.

Pia utaona faida ya kupungua kwa ulaji wa mafta wa gari lako hadi kwa asilimia 30% kulingana na ubora wa gari lako.

Teknolojia hii hufanya kazi kwa magari ya Petroli na Diesel na imejaribiwa na mamlaka za Japan kama Japan Automobile Transport Technology Association.

Miongoni mwa faida za mapema utakazozipata ni pamoja na:
  • Kuongezeka kwa msukumo wa gari( gari kuwa nyepesi)
  • Kuongezeka kwa spidi ya haraka
  • Kuwezesha gari kupanda mlima kwa ufanisi
  • Gari kuongezeka nguvu na engine kuwa smooth and silent


JINSI YA KUUNGANISHA ADPOWER KWENYE MFUMO WA GARI YAKO (VIDEO)




JINSI YA KUPATA ADPOWER YAKO

MAWASILIANO
Piga Simu: 0747 786 304
Whatsapp(bofya link): [(0747 786 304)

BEI ZA ADPOWER
Download Document ya Gharama: https://bit.ly/adpower-bei

PRICING-LIST-2 (2).png



AdPower Tanzania.

LFigAcGHcIRf9ePKj-DicCJ-_ovq0i-1B5rkBqWLlRRPYu_ORUrlRnXo7BJ86QSXxi3PLgwmpdo39XShBOpx9n2xUtXi0QJWSTzkouOKcPnCI57y0Tt5Z_wVjOMDXGYjGR_jFpcz



4ftSlVnFZhKfTkahWPFhH2nxPfTavqv9qAb4oyo04x140kXf8_6byDi7TBTyl_hGuLa2aJtGNIU10JyFgRTKf0-cAN6y6ehYnhxjtRhcjGMAv1uokE1nDZ57RBtif2_C_IbjzV6b
 
.... inafit kwenye kila aina ya gari (za kijapan)?
 
Inafiti kwenye gari aina zote Mkuu.
... shukrani; ngoja nifanye mchakato niagize. Kwenye required pieces sijaelewa vizuri; penye required pieces zaidi ya 1 maana yake ni lazima niagize kwa idadi iliyooneshwa? Nina kagari kamoja tu; ufafanuzi tafadhali.
 
... shukrani; ngoja nifanye mchakato niagize. Kwenye required pieces sijaelewa vizuri; penye required pieces zaidi ya 1 maana yake ni lazima niagize kwa idadi iliyooneshwa? Nina kagari kamoja tu; ufafanuzi tafadhali.
Yani ukishajua cc ya gari yako, unaangalia bei yake kule mwisho, kwahiyo bei unapewa package nzima, kama ni pieces 3 unapewa zote kwa bei hiyo. Sio kwamba kila piece inauzwa kwa bei hiyo, hapana ... Hiyo bei ni package nzima unapewa.
 
Yani ukishajua cc ya gari yako, unaangalia bei yake kule mwisho, kwahiyo bei unapewa package nzima, kama ni pieces 3 unapewa zote kwa bei hiyo. Sio kwamba kila piece inauzwa kwa bei hiyo, hapana ... Hiyo bei ni package nzima unapewa.
... asante sana kwa ufafanuzi. Kama nimeelewa gari inayohitaji 2 pieces maana yake zinafungwa zote kwa pamoja. Nimeelewa; thanks. Nitawapigia.
 
Acha utapeli ndugu. Hakuna faida kama hizo, huu ni wizi mtupu. Kusafisha/badilisha spark plugs kila mara pamoja na air filter vinatosha.

Eti unauza sticker kwa 750,000!

Wajinga ndiyo waliwao.
 
Acha utapeli ndugu. Hakuna faida kama hizo, huu ni wizi mtupu. Kusafisha/badilisha spark plugs kila mara pamoja na air filter vinatosha.

Eti unauza sticker kwa 750,000!

Wajinga ndiyo waliwao.


1.Angalia bei vizuri stika sio 750,000 ila idadi ya stika zinazohitajika ndio unazidisha na Tsh 75,000. Kwa gari ndogo ni Tsh 75,000

2. Hii teknolojia sio ya Tanzania na imekuwa imported from Japan ,na ipo pia amazon na Uk.

- Amazon product ASIN B01BSE8Q2K- https://www.amazon.co.jp/-/en/ADPOWER-PATENTED-Maintain-Performance-Maintenance/dp/B08Y1GSKM1
- Amazon product ASIN B08CBDJ2B8- https://adpower.opsfintell.co.uk/

3. Hii ni teknolojia moja miongoni wa teknolojia zilizopitishwa na kuidhinishwa na UN kama teknolojia zinazopunguza ulaji wa mafuta na ukaa. Angalia hapa
- Energy efficiency: Filtering Technology for Combustion Efficiency and Reducing Air Pollution | United Nations Industrial Development Organization
 
Amazon mtu yeyote anaweza kuuza chochote.

Hiyo link ya UN ni kwa product tofauti (spray), siyo hiyo sticker.

Kama hii teknolojia inakubalika sana, kwanini used cars karibia yote kutoka Japan hayana hii sticker kwenye air intake? Jibu ni,: Wajapani wenyewe hawajaikubali na ndiyo maana utaona kwenye website ya kampuni marketing ipo targeted nchi za dunia ya tatu kwenye wajinga wengi.
 
Ajabu sana huko Japan inakotengenezwa Amazon.co.jp wanasema "not currently available", lakini huku Tanzania wewe unafanya biashara.

Hata eBay, duka la adpower-global wamewauzia watu siyo zaidi ya 3 (watatu), na hawana stock.

 
Back
Top Bottom