Lidafo
JF-Expert Member
- Sep 26, 2019
- 889
- 1,789
"Mwanajeshi wa kweli anapambana sio kwa sababu anachukia kilichopo mbele yake, Ila ni kwa sababu anapenda kilichopo nyuma yake".
UTANGULIZI.
Natumai tu wazima na wenye shida na matatizo Mwenyezimungu awape sahali.
Nimeanza na msemo maarufu wa kijeshi unolenga kutoa maana ya ni nani mwanajeshi wa kweli, Hapa nitumie fursa hii Kueleza na kutoa maoni yangu juu ya Teknolojia na jeshi letu katika zama hizi ambazo nyuki wetu wamekosa uwezo wa kutengeneza asali.
Kwanza tufahamu maana ya teknolojia. Teknolojia Ni elimu inayohusu uhandisi, ufundi na ujenzi wa vifaa mbalimbali.
Ili uweze kuitekeleza teknolojia Ni lazima uhusishe maarifa ya sayansi.
Pili, Jeshi letu la wananchi wa Tanzania(JWTZ), Ni Jeshi ambalo kwa namna moja au nyingine linatumia teknolojia.
NI IPI DIRA YA JESHI LETU?
Dira ya jeshi la wananchi ni kuwa na jeshi dogo shupavu la viongozi na wataalamu wenye zana na silaha za kisasa, Utayari wa hali ya juu katika ulinzi wa nchi ya Tanzania(rejea www.tpdf.mil.tz ).
Sasa katika kuitekeleza dira hiyo jeshi letu linafanya kazi za kiuchumi, Kijamii, Shughuli za medani na pia limewekeza katika sayansi na teknolojia. Ila swali la msingi ni Je majeshi yetu yanafanya haya kwa kasi na kwa kiasi gani?, Je kiasi hicho na kasi hiyo ni sahihi kwa zama hizi?.
Katika kuyatafakari hayo tuangalie nguvu za majeshi ya nchi za wenzetu, Katika dunia hii majeshi yenye nguvu zaidi ni majeshi ya nchi za Urusi, Marekani, Korea Kaskazini, China na Izraeli, Sababu za majeshi hayo kuwa na nguvu ni uwezo wao wa kutengeneza silaha zao wenyewe (yaani wanamiliki teknolojia yao), wanauchumi mzuri na sera za hali ya juu za kijeshi.
Kama hizo ndio Sababu ,Sasa tujiulize majeshi yetu hayawezi kufika viwango hivyo?. Kwa mtazamo wangu jambo hili linawezekana sababu hata sisi tunaakili Kama wao, Hapa ashukuriwe mungu kwa kuwapa akili binadamu, Tatizo linakuja jinsi gani tunatumia akili zetu.
MIKAKATI ITAKAYOSAIDIA KUJIBORESHA KITEKNOLOJIA NA KULIONGEZEA NGUVU JESHI LETU.
Jeshi letu linaweza kujiboresha kiteknolojia kwa kufanya yafuatayo:-
KUWATUMIA VIJANA WA JKT MUJIBU WA SHERIA IPASAVYO.
Serikali iweke mpango wa kuwatumia vijana hawa, Wiki moja kabla ya kuhitimu mafunzo yao waiite wiki hiyo jina lokote mfano (wiki ya wazo chanya na teknolojia), Wawaweke vijana hawa katika makundi ya vijana ishirini ishirini kulingana na michepuo yao yaani wa sayansi na sanaa Kisha kila kundi lije na wazo, Maoni au ushauri juu ya jinsi gani tunaweza imarisha jeshi letu.
Faida za kutumia vijana wa mujibu wa sheria.
Serikali itaweza kukusanya mawazo ya vijana takriban 12000 kwa muda mchache, Kisha mawazo hayo yachujwe na wakuu wa makambi na kamati zao kisha yale bora ya wasilishwe Kamandi ya jeshi makao makuu kwa ajili ya kufanyiwa kazi , Naamini hatuwezi kukosa angalau mawazo matano mpaka kumi kwa kila operesheni ya kusaidia majeshi yetu na hata nchi yetu kukua kiteknolojia na hata kiuchumi
Ama kwa wale wanafunzi wa sanaa wataweza kulisaidia jeshi letu katika kuboresha na kuandaa sera nzuri zaidi. Baada ya hapo nyuki hawa watahitimu mafunzo yao huku wakiwa wameacha asali nyingi kwa ajili yao na vizazi vijavyo kuliko kuwaruhusu nyuki hawa waondoke bila kuacha athari yeyote.
KUTENGENEZA SILAHA ZETU WENYEWE.
Hapa tunaweza sema ni ndoto lakini hapana linawezekana ikiwa tu tutakuwa na nia ya dhati kulifanikisha hili.
Kwanza tujiulize tunahitaji nini kulifanikisha hilo, Kwa haraka haraka tunahitaji wataalamu na hapa sio lazima wawe wasomi tu bali hata watu wenye vipaji na vipawa katika ufanyaji, kutafakari na ufahamu wa maswala ya teknolojia, Pia tunahitaji fedha na maeneo ya wiwanda hili pia linawezekana .
Kwa kutumia mawazo ya maafisa wa jeshi na vijana wa JKT tutaweza kuingia katika utekelezaji huo.
Faida za kutengeneza silaha zetu wenyewe
Faida ni nyingi na za wazi kabisa, Kwanza kabisa serikali itaokoa fedha nyingi zinazotumika kununua silaha toka nje, Pili tutaiingizia Serikali pesa za kutosha kwa kuuza silaha kwa mataifa mengine hapa soko lipo kubwa sana hasa katika nchi jirani na Afrika kwa ujumla (Tuanze utekelezaji wa hili kabla jirani zetu hawaja amka.)
Nchi za mataifa yaliyoendelea waliwekeza katika sayansi na teknolojia na kufanya tafiti za kutosha juu ya uundaji wa silaha , Kwa mfano nchi za Israeli na China na Sasa wanaona matunda ya walichowekeza picha zifuatazo zinathibitisha Hilo.
Hiyo ni picha ya gari aina ya WZ551/ZSL92 lisilopenya risasi ambalo hutumika kuwaingiza wanajeshi katika uwanja wa vita limetengenezwa nchini China. (picha na maelezo kutoka Instagram page@militaryforcetz_).
Hiyo ni SMG aina ya UZI kutoka izraeli iliyogunduliwa mwaka 1948 na kuanza kutengenezwa mwaka 1950 nchini izraeli. (picha na maelezo kutoka Instagram page@militaryforcetz_).
Nimeweka hizo picha na hayo maelezo ili iwe chachu ya kutufikirisha akili zetu , Hapa tutafakari kwamba wenzetu wamewekeza bila kujali changamoto na muda wakupata matokeo.
Hivyo na sisi tukubali kuwa msingi na vizazi vijavyo, Tukiogopa sisi kuanza masuala ya kutengeneza silaha zetu na kukuza uchumi wetu sisi Kama watanzania, Maendeleo na ukuaji wa kijeshi tutayasikia kwa wenzetu, na hivyo kushindawa kuwatumia nyuki wetu kututengenezea asali kwa sababu tu ya kupumbazwa na utamu wa asali za nyuki wa koo za mbali.
Nimatumaini yangu sasa kuanza kuona serikali kupitia wizara yake ya ulinzi kwa kushirikiana na wizara ya Elimu sayansi na teknolojia kwa kutumia majeshi yetu wanaleta mapinduzi katika jeshi letu na kuliimarisha zaidi, Na hili litafikiwa kwa viongozi wetu tuliowapa dhamana kusimama imara kama mzinga wa nyuki na kuruhusu nyuki kuingia ndani na kutoka nje kwa lengo la kutengeneza asali yetu, Kuliko kuwapuuza nyuki hawa na kuwaacha jangwani pasina maji wala maua .
HITIMISHO
Makala hii ni kwa lengo la kuleta chachu katika kuelekea mabadiliko ya sayansi na teknolojia kijeshi, Ni vizuri kuona jeshi letu linaongoza katika tafiti na ugunduzi wa vitu mbalimbali nchini kwetu.
Mwisho, Nitoe pongezi kwa majeshi yetu kwa kazi nzuri wanayofanya ya kulinda mipaka yetu niwakumbushe kuwa wao ni katika tunu zetu. Mungu awatangulie katika kutekeleza majukumu yao.
Karibuni kwa maoni na mawazo mbalimbali juu ya mifumo na mbinu za kukuza jeshi letu katika mawanda ya sayansi na teknolojia.
Asanteni
Mwandishi Shafii R. Bakari (Lidafo).

Upvote
2