Teknolojia na Maisha: Je, tunakwenda wapi?

Abubakari Mussa

Senior Member
Joined
Mar 26, 2020
Posts
129
Reaction score
188
Habari Jamii!

Nimekuwa nikifikiria sana jinsi teknolojia inavyobadilisha jinsi tunavyoishi na kufanya kazi leo. Kutoka kwa simu zetu za mkononi hadi kwa matumizi ya AI, teknolojia inaingilia kati kila sehemu ya maisha yetu.

Nataka kuanzisha mjadala kuhusu athari za mabadiliko haya. Je, unadhani teknolojia inavyobadilisha maisha yetu kwa njia gani? Je, unayoona mabadiliko haya kama chanzo cha fursa au changamoto? Hebu tujadili jinsi teknolojia inavyoathiri kazi, mawasiliano, elimu, na hata uhusiano wa kijamii.

Ninafikiria, kwa mfano, jinsi teknolojia ya kazi ya mbali inavyobadilisha mawasiliano na muundo wa kazi, au jinsi AI inavyoathiri soko la ajira. Lakini pia, tuweze kutazama jinsi teknolojia inavyotoa fursa mpya za biashara, elimu, na hata kuleta mabadiliko katika jamii yetu.

Nina hamu ya kusikia maoni yenu! Hebu tushirikiane mawazo, uzoefu, na mtazamo wetu kuhusu mwelekeo wa teknolojia na jinsi unavyobadilisha maisha yetu.

Karibuni kwenye mjadala!
 
Teknolojia inakuwa na inaendelea kukua kwa kasi sana. Kwenye suala la ajira tunategemea kundi kubwa sana la watu kupoteza kazi

Na walioko kwenye janga kubwa la kupoteza ajira zao ni askari wa barabarani pamoja na Secretary kwa jinsi teknolojia inavyozidi kuwa hayo makundi mawili yanakuja kupotea kutokana na ukuaji wa teknolojia.

Vile vile ongezeko la wizi kwa mfumo wa mtandao. Hivyo tukubaliane tu na teknolojia ila tuendele kujiweka na kubadilika kulingana na mfumo wa maisha unavyoenda. Ni mtazamo tu ruksa kupinga.
 
Unaweza fafanua vizuri apo kwa askari na secretary?
Police ukimaanisha matumizi ya camera na kukatiwa fine kwa e-ways? Au yaani njia za mtandao tu? Shukran
 
Kuna teknolojia ya marobot inakuja kwa kasi kwa mfano traffic police baada ya kusimama barabarani root zitasimama badaya ya hao police traffic na hivyo hivyo kwa secretary.
 
Mi sionagi kama teknolojia inapoteza ajira za watu, Infact ni kweli kuna baadhi ya ajira hazittokuepo ila sio watu watapoteza kwasababu kutakuwa na ajira nyingi sana mpya zitakazotengenezwa ukilinganisha na zitakazotoweka. Watu wanaohofia kupoteza ajira zao wengi wao hawakocompetent kwenye sekta husika, kama kweli wewe ni mbobezi kwenye sekta yako teknolojia itakurahisishia zaidi kazi zako
 
Kuna baadhi ya maeneo upo competent lakini huwezi kuzidi uwezo wa tech kama AI na baadhi ya sehemu
Pia baathi ya tech haihusiani na competency, fikiria matumizi ya mitambo ya kunyanyulia vitu
Kwanza inapunguza cost, pili efficiency tatu mudaa , nk
Kwaio mimi naona tech itaathiri vitu vingi sana
 
Kuwa competent haimaanishi ushindane uwezo na AI, ukiwa competent kwenye field yako ni rahisi kuona opportunities technology inapoingizwa.
Fikiria before industrialization na baada ya industrialization ni wapi kumekuwa na ajira nyingi zaidi ???
Miaka ya nyuma dunia ilipoingia kweny uchumi wa viwanda watu walikosa kazi lakini angalia mpaka leo ajira ngapi mpya zimejitokeza kutokana na viwanda na machines??? Tena kwa Level ya civilization tuliyofikia saivi binadamu hakutakuwa na swala la kupoteza ajira kama ilivyokipindi kile zaidi ni ajira nyingi sana zitatokea.

AI will never replace humans in Job, Never Ever
 
Good point man
 
Back
Top Bottom