Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,547
- 7,167
Poleni na majukumu ya juma zima familia ya JF. Niende kwenye mada hapo juu. Ndugu zetu wakenya wamefanya uchaguzi lakini kura zilizotolewa kwa njia ya electroniki zimekataliwa na upinzani wakitaka zilizohesabiwa kwa mikono yaani majumuisho kwenye fomu namba 34A kutoka kila kituo cha uchaguzi. Wapinzani haohao walikataa mwanzoni kabla ya uchaguzi kura kuhesabiwa kwa mikono na walidai fomu huchakachuliwa na hazitoi matokeo halisi na badala yake itumike electroniki. Nakumbuka walienda hadi mahakamani kudai haki hii. Leo wamebadilika. Je tujifunze nini kama Watanzania kupitia mbinu hizi mbili za kuhesabu kura?